Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza Mwakilishi
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Alberic Kacou kufuatia
Umoja wa Mataifa kutimiza Miaka 67 tokea kuasisiwa kwake. Pongezi hizo
amezitoa Ofisini kwake katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo
Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mwakilishi
Mkazi wa Umoja wa Mataifa aliyepo Tanzania Bw. Alberic Kacou
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi
Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi Mpya wa Shirika la Mpango wa
Maendeleo la Umoja wa Mataifa Zanzibar Bibi Anna Senga.Kulia ni
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bwana Alberic
Kacaou na kushoto kwa Balozi Seif ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohd.
---
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameupongeza Umoja wa
Mataifa (UN) kwa kutimia miaka 67 tokea kuasisiwa kwake mnamo mwaka
1945.
Balozi
Seif ametoa pongezi hizo wakati akisalimiana na Ujumbe wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Ofisini kwake katika
Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Ujumbe
huo wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa ulioongozwa
na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa aliyepo Nchini Tanzania Bw.
Alberic Kacou uliambatana pia na Mwakilishi wa Shirika hilo aliyepo
Zanzibar Bibi Anna Senga.
Balozi
Seif amesema Umoja huo umeundwa maalum kwa lengo la kutoa huduma
itakayokidhi mahitaji ya Mataifa yote Wanachama wa Umoja huo hasa
katika masuala ya kustawisha Amani na ustawi wa Jamii.
Ameeleza
kwamba Taasisi zilizoundwa chini ya mwavuli wa Umoja huo zimekuwa
zikiendelea kutoa huduma mbali mbali kwa Mataifa Wanachama zilizopelekea
kupiga hatua kubwa za Maendeleo hasa katika Nchi za Dunia ya Tatu.
Amesema
Jamii za Kimataifa zimekuwa zikishuhudia ufanisi huo hasa katika miradi
ya Afya, Chakula na lishe, Maji, sambamba na kudhamini Mafunzo ya Elimu
ya Uraia kwa lengo la kutandika Demokrasia Duniani.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameueleza Ujumbe huo wa Shirika la Mpango
wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa kwamba Zanzibar bado inahitaji
kuendelea kuungwa mkono na Taasisi za Umoja huo katika harakati zake za
Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
Amefahamisha
kwamba mradi wa huduma za maji safi na salama katika maeneo mbali mbali
ya Visiwa vya Unguja na Pemba umepewa kipaumbele katika jitihada za
kuweka miundo mbinu.
Mapema
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa aliyepo Nchini Tanzania Bw.
Alberic Kacou alimueleza Balozi Seif kwamba Umoja huo kupitia Mashirika
yake ya Umoja huo (UNDP) yatajitahidi kuendelea kuangalia mazingira ya
kusaidia sekta ya Afya, Chakula na Lishe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)