Meneja wa Benki ya NMB tawi la Songea Rehema Nassib (kushoto) akimkabidhi Kaimu Afisa Elimu ya Msingi Wilaya ya Songea vijijini,Vicent Kayombo moja ya madawati 80 yaliyotolewa na Benki hiyo ikiwa ni msaada kwa ajili ya shule 4 za msingi katika jimbo la Peramiho.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Songea Rehema Nassib akingumza mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati 80 kwa ajili ya shule nne za msingi katika jimbo la Peramiho.Katikati ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini,Thomas Kilongo na Kulia ni Kaimu Afisa Elimu ya Msingi Wilaya ya Songea vijijini,Vicent Kayombo.
Kaimu Afisa Elimu ya Msingi Wilaya ya Songea vijijini,Vicent Kayombo akingumza mara baada ya wilaya hiyo kupokea msaada wa madawati 80 kutoka kwa Benki ya NMB tawi la Songea kwa ajili ya shule nne katika jimbo la Peramiho.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ngadinda,John Komba (aliesimama) akitoa shukurani baada ya kijiji chake kupata msaada wa madawati 20 kwa ajili ya shule ya msingi Sokoine iliyopo katika kijiji hicho yaliyotolewa na Benki ya NMB tawi la Songea.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Sokoine kijiji cha Ngadinda halmshauri ya songea vijijini wakibeba madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB tawi la Songea,ikiwa ni msaada kwa shule hiyo ambapo ilitoa msaada wa madawati 80 kwa shule nne katika jimbo la Peramiho.
PICHA NA MUHIDIN AMRI WA GLOBU YA JAMII - RUVUMA.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)