Meneja
wa NMB Kanda ya Ziwa , Straton Chilongola akiwasalimia wanafunzi wa
Shule ya Msingi Sota iliyopo Rorya mkoani Mara, baada ya kuwakabidhi
madawati, meza pamoja na viti nyenye thamani ya shilingi milioni tano.
Meneja
wa NMB Kanda ya Ziwa, Straton Chilongola (kushoto) akikabidhi moja ya
madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa mkuu wa Shule ya
Msingi Muungano , Maswali Buyunge ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa
na NMB kwa shule hiyoWanafunzi
wa Shule ya Msingi Muungano iliyopo kijijini Kirejeshi ,wilaya ya
Busega mkoani Simiyu, wakiwa wameketi katika baadhi ya madawat 50
waliyokabidhiwa na benki ya NMB ikiwa ni msaada wa benki ya NMB kwa
shule hiyo..
Meneja
wa benki ya NMB Rorya, Penina Kiranga ( kati) akikabidhi vifaa ikiwa
ni sehemu ya madawati 50, meza 19 pamoja na viti 19 vyenye thamani ya
shilingi 5 milioni kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sota Bw.Steven
Dhaje (pili kushoto) iliyopo Rorya, Mara. Wakishuhudia ni Meneja wa
NMB Kanda ya Ziwa, Straton Chilongola, (Kulia) Afisa wa benki na Mwalimu wa Shule hiyo.
Meneja
wa NMB Kanda ya Ziwa, Straton Chilongola (kushoto) akikabidhi moja ya
madawati 100 yaliyotolewa na NMB yenye thamani ya shilingi milioni 5
kwa Afisa Elimu wa wilaya ya Busega, Mwita Chogoro kwa ajili ya Shule
za Msingi Muungano, Nyamatembe na Mwamkinga ikiwa ni msaada uliyotolewa
na benki ya NMB.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)