Aswin Rana, Chairman Speaking
Participant atended Conference TSPA,
Deputy Minister for, Agriculture and Food Security,(FSSP)
Adama Malima addreses whe the opening the Conference, Federation Of
SADC Sugar Producers held Dar es Salaam Kunduch Beach Hotel
Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema nchi
inakabiliwa na uhaba wa sukari tani 150,000 kila mwaka kutokana na uwezo wa
viwanda hapa nchini kuzalisha tani 350,00 wakati mahitaji ni tani 500,000 kwa
mwaka.
Hayo
yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima
alipokuwa akifungua mkutano wa wazalishaji wa sukari kutoka nchi za Jumuiya ya
Uchumi Kusini mwa Africa(SADC), unaoendelea jijini Dar es Salaam Malima
alisema kiasi hicho ambacho ni pungufu imekuwa ngumu kukipata kutoka nchi
nyingine kwa kuwa nazo zinahitaji sukari kwa wingi.
“Sisi
hatuzalishi sukari kwa kiwango cha kutosha, tuna mahitaji ya sukari tani laki
tano kwa mwaka sisi tunazalisha tani laki tatu na hamsini hivyo tuna uhaba wa
tani laki moja na nusu ambayo nayo ni ngumu kuipata kutoka kwa wenzetu,”alisema
Malima.
Alisema
kutokana na hali hiyo Serikali inaweka mkakati ya kutaka uzalishwaji wa sukari
ufikie tani milioni moja kwa mwaka ndani ya miaka sita ijayo.
“Kutokana
na hilo wadau wa sekta hii ni muhimu wakajipanga ili kuhakikisha lengo hilo
linatimia,”alisema na kuongeza;
“Tunaangalia
maeneo muhimu ya uzalishaji wa miwa ambayo ndiyo inatumika kutengeneza sukari
ili kufanikisha hilo.”
Katibu
Mtendaji wa Taasisi ya Wazalishaji wa Sukari Tanzania(TSPA), Balozi Fadhili Mbaga alisema kwa mwaka
huu wanategemea kuzalisha sukari kiasi cha tani 320,000 kwa kuwa msimu ni
mzuri.
“Mwaka jana tulizalisha tani 80,000
ambayo ilikuwa ni kidogo ila mwaka huu tunatarajia kuzalisha kiasi kikubwa
ambacho bado kitakuwa hakitoshi kwa matumizi ya hapa nchini,”alisema Balozi
Mbaga.
Alisema
hivi sasa nchi za SADC zinazalisha wastani wa tani milioni tano za sukari kwa
mwaka ambayo ni asilimia 3 ya uzalishwaji wa sukari duniani.
Mkutano
huo umehudhuriwa na nchi ya Angola, Botswana,
Lesotho, Malawi, Mauritius, Musumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland,
Tanzania, Zambia na Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)