Mratibu
wa Mradi wa chama cha wakutubi kutoka Finland (TLF) Marjatta Lahthi
akitoa taarifa yake katika ufunguzi wa mkutano wa maktaba kwa
maendeleo jijini Dr es Salaam leo ambapo umewashirikisha zaidi ya watu
80 wakiwemo wadau wa maktaba pamoja na wajasiriamali kutoka Tanzania,
Kenya,Finland,Gemany, Italy na United Kingdom. Mradi huo kupitia
maktaba pamoja na mtumizi ya teknolojia ya ICT utawawezesha kupata
habari mbalimbali za shughuli zao za kila siku.
Mkurugenzi
Mkuu wa TLSB Dkt. Alli Mcharazo akitoa taarifa yake wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa Maktaba kwa maendeleo leo jijini Dar es Salaam ambao
umefunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Selestine Gisimba (hayupo pichani).
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa Libraries for Development wakiwa katika
mkutano huo wa siku mbili uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Selestine Gisimba (hayupo pichani )
leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umewashirikisha washiriki wapatao
80 kutoka nchi ya Tanzania, Kenya, Finland, Germany, Italy na United
Kingdom. Mradi huo wa Maktaba kupitia teknolojia ya ICT utawawezesha
kuwasaidia kupata elimu na taarifa mbalimbali za shughuli zao za kila
siku.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Libraries for Development wakiwa
katika mkutano huo wa siku mbili uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Selestine Gisimba (hayupo pichani )
leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umewashirikisha washiriki wapatao
80 kutoka nchi ya Tanzania, Kenya, Finland, Germany, Italy na United
Kingdom. Mradi huo wa Maktaba kupitia teknolojia ya ICT utawawezesha
kuwasaidia kupata elimu na taarifa mbalimbali za shughuli zao za kila
siku.
Washiriki wakikagua vitabu.
Picha ya pamoja. Picha zote na Mwanakombo Jmaa-MAELEZO





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)