Pichani
Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt.
Alberic Kacou akizungumza machache kuhusiana na umuhimu wa wiki ya Umoja
wa Mataifa inayoanza leo, ambapo amesema mabadiliko ya hali ya hewa
yanayotokea duniani ni ushahidi wa kutosha wa ongezeko la mafuriko na
ukame kunakotokana na uharibifu wa mazingira mambo ambayo tunapaswa
kuyachukulia kama changamoto kwa kuwa yanatukwaza katika kutimiza
malengo ya Maendeleo ya Milenia.
Ameongeza
kuwa Wiki ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2012 inaadhimishwa kwa shughuli
mbalimbali zinazolenga vijana, wanafunzi, wasomi, vyombo vya habari na
jamii kwa ujumla.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John
Haule akizungumzia maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa ambapo
pamoja na mambo mengine amesema kutakuwa na maonyesho yatakayofanyika
katika viwanja vya Karimjee siku ya tarehe 23 na 24 mwezi huu ambapo
wananchi wataona mipango na miradi mbalimbali ambayo Umoja wa mataifa
umekuwa ukiisaidia Tanzania na pia amesema kutakuwa na mjadala wa wazi
katika ukumbi huo siku ya tarehe 23 ambapo wananchi wanakaribishwa
kushiriki na kutoa mawazo yao.
……………………………………………………..
Na.Mwandishi wetu
Tanzania
inaungana na nchi nyingine mbalimbali duniani kuadhimisha miaka 67 ya
Umoja wa Mataifa ambapo kutakuwa na shughuli mbali mbali zinazoanza leo
tarehe 17 mpaka siku ya tarehe 24 Oktoba ambayo ndio siku ya kilele cha
shughuli hizo.
Kitaifa
nchini Tanzania miaka 67 ya Umoja wa Mataifa itaadhimishwa kwa kauli
mbiu ambazo zimekuwa zikitoka kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni
‘Changing Peoples’ Lives: Greening The Environment For Sustainable
Livelihoods’.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule amesema kauli mbiu hiyo
imekuja wakati muafaka ili kutukumbusha mahusiano yetu ndani ya Jumuiya
ya Umoja wa Mataifa lakini vilevile inatukumbusha changamoto ya jinsi
uharibifu wa mazingira unavyofanyika hivi sasa.
Ameongeza kuwa wiki ya maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa itaadhimishwa na matukio mbali mbali ikiwemo uzinduzi wa leo, na Siku ya Familia itakayohusisha michezo mbali mbali itakayofanyika kwenye viwanja wa Leaders Club tarehe 20 Oktoba 2012.
Ameongeza kuwa wiki ya maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa itaadhimishwa na matukio mbali mbali ikiwemo uzinduzi wa leo, na Siku ya Familia itakayohusisha michezo mbali mbali itakayofanyika kwenye viwanja wa Leaders Club tarehe 20 Oktoba 2012.
Michezo
hiyo itawahusisha wanadiplomasia waliopo nchini Tanzania, wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)