Malori yanayobeba Udongo katika
eneo la Ujenzi yakiingia na kutoka wakati wa usiku huku yakiwa
hayajafunikwa na maturubai hali inayosababisha kumwaga udongo katika
barabara za jiji na kusababisha uchafuzi unaolalamikiwa na kampuni
zinazofanya usafi.
Bango la Mkandarasi anayejenga
jengo hilo lililopo kwenye kiwanja namba 01 katika makutano ya Barabara
ya Ali Hassan Mwinyi na Ufukoni jijini Dar es Salaam ambapo linaonyesha
Wajenzi ni Kampuni ya China Railway Jiachang Engineering Co. Ltd.
Moja ya Malori ya mchanga likitoka baada ya kuzoa udongo katika jengo hilo na kujazwa kupita kiasi.
Muonekano wa uchafu katika
barabara kutokana na kumwagika kwa udongo unaosombwa na malori hayo
ambao unapelekea kuziba kwa mitaro na kuchakaza lami.
Malori yakiwa kwenye foleni ya kuzoa udongo katika jengo hilo.
Na.Mwandishi wetu
Tunapozungumzia Suala la usafi wa Mazingira kwa asilimia kubwa ya wanajamii wanaelewa maana yake na umuhimu wake.
Na tunapozungumzia kutunza usafi
katika mazingira yetu tunamaanisha kuanzia tunapoishi hadi katika
barabara za ndani na zile kubwa za lami zinazotumika mijini.
Wote tumeshuhudia Manispaa ya Ilala
ambayo ndio kitovu cha jiji la Dar es Salaam, ikizindua kampeni za
kufanya usafi katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na katika barabara
kubwa za jijini.
Katika kutimiza malengo hayo kampuni ya ‘Green Waste Pro Ltd’ ikafanikiwa kushinda zabuni ya kufanya usafi katika manispaa hiyo.
Ama kwa hakika kapuni hiyo yenye
magari ya kutosha likiwemo gari la kisasa la kupiga deki barabara,
ikaanza kazi hiyo na kipindi kifupi matokeo yakaaanza kuonekana.
Sasa basi katika kile kinachoonekana
ama kutojali au kupuuzia taratibu za usafi kampuni moja iliyopewa
kandarasi ya kujenga jengo moja katika ene la mtaa wa Ufukweni jiji Dar,
imekuwa ikichafua mazangira ya jiji bila kujali.
Mpiga picha wetu ameshuhudia magari
makubwa ya kampuni hiyo yakibeba udongo nyakati za usiku huku yaendeshwa
hovyo na kumwaga udongo huo barabarani na kuacha vumbi likitimka
hewani.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Gree
Waste Pro Ltd’ Bw. Mac Antony Shayo amesema, kwa kawaida magari
yanayofanya shughuli hiyo yanapswa kusafishwa pale pale kwenye saiti
kabla ya kutoka nje, ili kuepuka kuchafua mji.
Ameongeza kusema kuwa kingine ni
kwamba magari hayo yanajazwa sana udongo kuliko kiwango kinachoshauriwa
na pia hayafunikwi, hivyo yanaacha tu matope barabara yote kuanzia
yanakotoka, na mbaya zaidi yanaingia ‘City Centre’.
Amesema kuwa utaratibu huo sio sahihi
na gharama zinazotumika kusafisha barabara ni kubwa na kinachojitokeza
kwa sasa ni kwamba Manispaa inajitahidi kufanya usafi wao wanakazana
kuchafua.
Bw. Shayo amesema pamoja na kuchafua
barabara pia ndio chanzo cha uharibifu wa lami, na pia udongo kujaa
katika mifereji kipindi cha mvua.
Aidha amesema kampuni hiyo inapaswa
inyimwe kuendelea na kazi hiyo mpaka itakaporekebisha taratibu zao za
utendaji ikiwemo kusafisha hayo magari yao ili yaweze kubeba uchafu kwa
njia ya usafi.
Alifafanua kuwa, gari hizo zisijazwe
na zifunikwe kama sheria inavyotaka kwa kuwa sheria haikuwekwa ili mtu
asimamiwe bali imewekwa ili itekelezwe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)