MSANII wa chimbo la filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima. Usiku wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa Ommy Dimpoz, Chidy Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic. Habari/Picha: Musa Mateja/GPL





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)