Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Lyimo Barlow AZIKWA NYUMBANI KWAKE MOSHI MKOANI KILIMANJARO JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Lyimo Barlow AZIKWA NYUMBANI KWAKE MOSHI MKOANI KILIMANJARO JANA

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,Mh PEREIRA SILIMA, akiweka shada la Maua kwa aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,Liberatus Lyimo Barlow mara baada ya kuzikwa jioni ya jana kijijini kwao Kilema Kyou,Wilaya ya Moshi vijini Mkoani Kilimanjaro,mara baada ya mazishi hayo kufanyika.Aidha mazishi hayo yamehudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo, viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini pamoja na wale wa vyama vya Kisiasa hapa nchini. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema  akiweka shada la Maua kwa aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,Liberatus Lyimo Barlow mara baada ya kuzikwa jioni ya jana kijijini kwao Kilema Kyou,Wilaya ya Moshi vijini Mkoani Kilimanjaro,mara baada ya mazishi kufanyika.Aidha mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini pamoja na wale wa vyama vya Kisiasa hapa nchini.
Mke wa marehemu nae akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mumewe
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema  akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa jiji la Mwanza,Mhe.Eng. Evarist Ndikilo  
 Sanduku lenye mwili wa marehemu likiingizwa kwenye nyumba yake ya milele.
 sehemu ya umati wa watu wakiwemo maofisa mbalimbali wa jeshi la polisi.
 Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,Mh PEREIRA SILIMA akitoa heshima zake za mwisho mapema leo kwenye mazishi ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,Liberatus Lyimo Barlow  kijijini kwao alikozaliwa Kilema Kyou,Wilaya ya Moshi vijini Mkoani Kilimanjaro.KWA PICHA ZAIDI YA TUKIO HILI BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages