ZAIDI YA WATEJA 500 WA NMB WAJISHINDIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ZAIDI YA WATEJA 500 WA NMB WAJISHINDIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB

Meneja wa Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi, Julius Konyani akibonyeza kitufe kuwatafuta washindi wa promosheni ya mwisho ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika jijini Dar es Salaama. Wa pili kushoto, Ofisa kutoka Selcom, Everline Simpilu na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhusein.

Na Salum Mkandemba

BENKI ya NMB, imewazawadia washindi wa bahati nasibu yake ya Jenga Maisha na NMB, wakiwamo wanne walioshinda Tani Moja moja ya saruji, mmoja akijishindia Mabati ya Kuezekea, mwingine Amana Maradufu na wengine 20 wakijishindia Mabegi ya Shule.

Katika promosheni ya mwisho iliyodumu kwa miezi mitatu, wateja wa benki hiyo wenye NMB Bonus Account na NMB Junior Account walikuwa walengwa waliopata nafasi za kushiriki na kujishindia zawadi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa droo ya kuwapata na hatimaye kuwatangaza washindi hao, Meneja Mahusiano wa Huduma kwa Wateja Binafsi, Julius Konyani, alisema kuwa NMB iliamua kufanya bahati nasibu hiyo kama jitihada zao katika kuunga mkono harakati za wateja wake.

“Utafiti wa NMB unaonesha kuwa, wateja wengi ufungua akaunti zao kwa nia ya kutimiza malengo yao kama vile kujenga nyumba, kusomesha watoto nk, nasi kwa kuwajali wateja wetu wa NMB Bonus Account na NMB Junior Account tukaanzisha shindano hili,” alisema Konyani.

Droo hiyo ilishuhudiwa na Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka bodi ya michezo hiyo nchini Humud Abdulhussein, ambapo Annania Alfred Nyanza wa Kasulu na Nemima Joel Mbwana, walitangazwa miongoni mwa washindi wanne wa tani moja moja ya saruji.

Kwa upande wa zawadi ya mshindi wa Mabati ya Kuezekea, Mwanahawa Selemani Mwamoja wa Kilwa aliibuka mshindi, huku Libaba Mohammed Juma wa Nachingwea akijishindia zawadi ya Amana Maradufu, itakayowezesha kutunisha akaunti yake mara mbili.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages