Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dr. Emmanuel Nchini akipokea vifaa vya kupimia ulevi kwa madereva kutoka kwa Steve Gannon mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani, vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 60, katika msaada huo pia kampuni ya bia ya Serengeti imetoa vitabu 20000 vya leseni kwa ajili ya kusaidia wiki ya nenda kwa usalama barabarani inayotarajiwa kuzinduliwa siku ya jumatatu mkoani Iringa kitaifa, kushoto ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akitambulisha viongozi mbalimbali katika hafla ya makabidhiano ya vifaa maalum vya kupimia ulevi kwa madereva, wa pili kutoka kulia ni Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi, kulia Katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani Mbarak Abdulwakil na katikati ni Steve Gannon mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL).
Steve Gannon mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL) akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, katikati ni Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi, kulia Katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani Mbarak Abdulwakil.
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga akijaribu jinsi ya kutumia kifaa hicho huku Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi, kulia Katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani Mbarak Abdulwakil wakiangalia, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda na Steve Gannon mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)