Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Peter akipata maelekezo ya namna ya kupiga kura yake
kutoka kwa Meneja wa Tawi la Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) Arusha Bw.
Wily Lyimo muda mfupi kabla ya kupiga kura yake katika kituo cha
Mikutano cha AICC mjini Arusha hivi karibuni.
……………………………………..
Na: Geofrey Tengeneza
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo
Pinda hivi karibuni amepiga kura yake ya kuvichagua vivutio vitatu vya
Tanzana katika shindano linaloendelea hivi sasa la kutafuta maajabu Saba
ya asili ya Afrika.
Waziri Mkuu alipiga kura yake
wakati wa mkutano wa tano wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF
uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa AICC mjini Arusha
ambapo Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iliweka kituo cha kupigia kura kwa
njia ya mtandao wa komputa (internet). Waziri Mkuu alivipigia kura
vivutio hivyo vitatu ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti na Kreta ya Ngorongoro ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu
Saba ya Asili barani Afrika. Viongozi wengine waliopiga kura zao wakati
wa mkutano huo katika kituo hicho cha Bodi ya utalii Tanzania ni pamoja
na Waziri wa Kazi na Ajira Mh.Gaudensia Kabaka, Naibu Waziri wa
TAMISEMI Mh.Henry Mwanri na viongozi mbalimbali wa LAPF.
Bodi ya Utalii Tanzania hivi sasa
inaendesha kampeni kamambe ya kuwahamasisha watanzania kuvipigia kura
vivutio hivyo, na katika mkutano huo iliamua kupiga kambi katika kituo
hicho cha mikutano ya Kimataifa cha AICC kwa lengo la
kuwahamashishawajumbe wa mkutano huo na kuhakikisha wale ambao
hawajapiga kura wanapiga kura zao katika kituo hicho hapo AICC zoezi
ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Tanzania ni nchi pekee barani Afrika iliyoingiza vivutio vingi katika shindano hilo ambapo imefanikiwa kuiongiza vivutio vitatu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)