Na Elizabeth John
MASHINDANO ya gofu ya
kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere ya NMB Nyerere Masters yanatarajiwa kufanyika
Oktoba 13 hadi 14 mwaka huu katika viwanja vya Gymkhana.
Mashindano hayo ambayo
yanafanyika kila mwaka, yakiwa na lengo la kumuenzi muasisi wa taifa hili na
rais wa kwanza wa Tanzania,
Mwalimu Nyerere yanadhaminiwa na Benki ya NMB.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
leo, Katibu Tawala wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Sophie Nyanjera alisema
benki hiyo imedhamini zawadi za washindi katika kila kipengele ambazo ni fulana
na kofia pamoja na kusaidia shughuli nyingine za mashindano hayo.
Nyanjera alisema mashindano
hayo yatakuwa ya aina yake kutokana na klabu zote za Tanzania Bara kuleta
wawakilishi wao.
“Matarajio yetu ni klabu zote
kushiriki ili mashindano yawe na ushindani mkubwa ukizingatia zawadi za mwaka
huu ni nzuri zaidi, hivyo muda bado upo kwa wale ambao hadi sasa
hawajadhibitisha kushiriki, wanatakiwa kufanya hivyo haraka,” alisema Sophie.
Alisema mashindano yatakuwa
na kiingilio cha sh. 30,000 kwa kila mchezaji, na kuwataka wachezaji wa kulipwa
pia kushiriki ili kuleta ushindani zaidi kwa wachezaji wa ndani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)