



Waweza
dhani watu hawa wapo katika foleni ya kupiga kura au kusubiri
kujiandikisha kwaajili ya vitambulisho vya Utaifa..la hasha bali foleni
hii ndefu ambayo huanzia majira ya alfajiri hadi usiku wakati mwingine ni ya baadhi ya wakazi wa Ukonga jijini Dar es Salaam waliojipanga jana kupata huduma ya LUKU.
Tangu
Septemba 1, 2012 Shirika la Ugavi la Umeme Tanzania (TANESCO)
waliutangazia umma wa Watanania kuwa kutaanza zoezi la uboreshaji wa
mfumo wa LUKU nchini. Kuanza kwa zoezi hili kumefanyika huku wananchi
wakipata adha kubwa ya kukaa katika foleni kwa muda mrefu na wengine
kukata tamaana kulala gizani katika nyumba zao.
Hali
hii hasa ina lalamikiwa kutokana na Shirika hilo kuwa na vituo
vichache vya kuuzia umeme jijini Dar es Salaam na nchi nzima kwa
ujumla. Hivyo shirika halina budi kuongeza pia vituo.Picha Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blog





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)