Makamu
wa Rais wa chama cha wafanyabiashara wa Uingizaji na Usafirishaji
wa dawa na vifaa tiba kutoka China (CCCMHPIE) Meng Dongping,
akizungumza katka mkutano wa wafanyabiashara wa Uingizaji na
Usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka nchini China Uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam. Amesema Tanzania ni nchi ya 11 katika ushirikiano wa
kibiashara wa bidhaa hizo barani Afrika na nchi ya pili kwenye soko la
bidhaa hizo wa nchi za EAC. ambapo katika kipindi cha miezi 6 cha mwaka
2012 ukuaji wa soko la bidhaa hizo nchini Tanzania umefikia dola za
Marekani milioni 32.61 sawa na asilimia 47. Picha na Mwanakombo
Jumaa-MAELEZO
Mdau
wa mkutano huo kutoka (MSD ) nchini, Cosmas Mwaifani, akiwasilisha mada
yake katika mkutano huo wa siku moja jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kuleta dawa
na vifaa tiba kutoka kwa wafanyabiashara wa uingizaji na usafirishaji
wa madawa na vifaa tiba kutoka China wakifuatilia mada mbalimbali
katika mkutano huo wa siku moja jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)