Mbunge
wa Iringa mjini, Peter Msigwa (mwenye magongo) akisalimiana na wadau
mbalimbali wa Usalama Barabarani, baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Samora mjini Iringa, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama
Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim ‘Asas’ Abri (kulia) Father Kidevu
(mwenye kofia) na Mdau Frank wa mjini Iringa. Pia Mbunge wa Viti Maalum
(CCM) Mkoa wa Iringa, Ritha Moto Kabati naye pia alipata wasaa wa kutembelea maonesho hayo.
Licha
ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini (CHADEMA) Rev. Peter Msigwa
kuuguza mguu wake kulia uliotenguka lakini alipata wasaa wa kuungana na
wananchi wa jimbo lake na taifa kwa ujumla kutembelea mabanda ya
Maonesho yaliyopo katika Uwanja wa Michezo wa Samora mjini Iringa
kujionea shughuli mbalimbali za Jeshi la Polisi na Vikosi vingine na
mabanda ya wadau wa Usalama Barabarani yaliyopo uwanjani hapo katika
maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa yanayofanyika Mkoani
Iringa ndani ya Jimbo lake. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni
“PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.

Mbunge Msigwa alisalimiana na watu mbalimbali wa eneo la Mlendege waliomlaki mara baada ya kuwasili. Picha na Mh. Peter Msigwa Blog





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)