Jakaya
Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akimpokea Rais Armando
Guebuza wa Msumbiji baada ya kuwasili leo Septemba 3, 2012 katika uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, tayari
kwa mkutano wa Troika ya SADC unaotarajiwa kufanyika kesho Septemba 4,
2012 katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi wajumbe
wa Asasi hiyo ambao ni Msumbiji ambao ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC,
Afrika Kusini aliyekuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo kabla ya Tanzania,
Namibia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi hiyo ya Troika, pamoja na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao ni wageni waalikwa.
Rais Armando Guebuza wa Msumbiji akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete
Rais Armando Guebuza wa Msumbiji akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete
Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akimuonesha
Rais Armando Guebuza wa Msumbiji mandhari ya Bandari ya Dar es salaam
kutoka katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, baada ya kuwasili leo
Septemba 3, 2012 tayari kwa mkutano wa Troika ya SADC unaotarajiwa
kufanyika kesho Septemba 4, 2012 hotelini hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi wajumbe
wa Asasi hiyo ambao ni Msumbiji ambao ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC,
Afrika Kusini aliyekuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo kabla ya Tanzania,
Namibia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi hiyo ya Troika, pamoja na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao ni wageni waalikwa. PICHA NA IKULU






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)