TASWIRA ZA Spika Makinda BAADA YA KUWASILI NCHINI ITALIA KWENYE MKUTANO WA MAKAZI WA ULIMWENGUNI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TASWIRA ZA Spika Makinda BAADA YA KUWASILI NCHINI ITALIA KWENYE MKUTANO WA MAKAZI WA ULIMWENGUNI

Spika Makinda katikati pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi Italia: kutoka kushoto ni Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Napoli ambaye makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Napoli Italia Bi Fatma Tandika, Mwenyekiti wa jumuiya ya watazania wanaoishi Napoli, Balozi wa Tanzania nchini Italia Dkt. James Nsekela na Afisa mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia Bw. Msemo
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akiwasili katika uwanja wa ndege wa Napoli, Italia na kulakiwa na mwenyeji wake, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dkt James Nsekela leo. Mhe. Makinda yuko nchini Italia kuhudhuria mkutao wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa unaohusu jinsi ya kukabiliana na ukuaji wa miji ulimwenguni. Hivyo zinahitajika juhudi za makusudi ili kuweka mipangilio stahihiki katika miji ya Tanzania hususan majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji. Ni hivi majuzi ilitangazwa kuwa Dar es Salaam ni miongoni mwa miji inayokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika. Ujumbe wa Tanzania katika mkjutano huu unaongozwa na naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Goodluck Ole Medeye.Mkutano huo utaanza kesho tarehe 2 na kuhitimishwa tarehe 6 septemba 2012.Picha na mdau Prosper Minja-Bunge

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages