
Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Tasilimu akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) mkataba wa Jumuia ya Afrika
Mashariki ambao wataufanyia kazi katika kikao cha Bunge kinachotarajia
kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya. Wabunge hao waliongea na
waandishi wa habari jana katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari
(Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Angela Kiziga ambaye
ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira
akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam kuhusu tofauti ya kiuchumi na maendeleo baina ya nchi tano
wanachama wa jumuia hiyo .

Katibu
wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji
(kulia) akiongea jambo na Abdullah Mwinyi (kushoto) ambaye ni Mjumbe wa
kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge hilo wakati wa mkutano baina yao
na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa
Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Vikao vya Bunge hilo
ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini
Kenya

Mwenyekiti
wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam
Kimbisa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na
kuviomba vyombo vyao viweze kutambulisha timu ya wabunge hao tisa kwa
watanzania ili wapate kuwafahamu kama wawakilishi wao wanaosimamia
masuala ya taifa. Kulia ni Mbunge Angela Kiziga ambaye ni Mwenyekiti wa
kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira katika bunge
hilo.Picha na Habari Maelezo





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)