Baadhi ya wasanii wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(TaSUBa) wakitoa
burudani wakati washerehe za mahafali ya 23 ya taasisi hiyo
zilizofanyika leo katikaukumbi wa maonesho ya taasisi hiyo.
Mtoto mwenye umri wa miaka 4 Nyambuli
Mganga akiwa na kikundi cha sanaa na utamadunikijulikanacho kwa jina
la Utandawazi Theatre Group MatwighaChalo kutoka Nansole Ukerewe
akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ukerewe inayojulikana
kwajina la Obusimbula katika meza kuu ,ambaye amekuwa kivutiokutokana
na kucheza kwake mwenyewe bila kuelelezwa wakati maonesho ya 31 ya
Tamasha na Sanaa na Utamaduni liliyofanyika katika Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni (TAsuBA) iliyopo Bagamoyo, mkoa wa Pwani ,. Nyambuli ambaye
anarithi utamaduni huo kutoka kwa mama yake, Wiliherimina Kebela .
Maonesho hayo yamaeambatana na Sherehe za mahafali ya 23 yataasisi
hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mwenyekiti wa Bodi
ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni(TaSuBa), Profesa Elias Jengo ambaye ni Mhadhili
wa taaluma hiyo katika Chuo Kikuu cha Dares Salaam(UDSM),akimpatia cheti
mhitimu wa Stashada ya Sanaa na Utamaduni , Charles Kiswaga katika mahafali ya
23 ya yaliyofanyika kwenye ukumbi wa maonesho chuoni hapo. Katikati Mtendaji
Mkuu wa taasisi hiyo Juma Bakari na kulia ni Mkuu
wa Idara ya Taaluma Michael Kadinde.
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada ya Juu ya Sanaa na Utamaduni wakiwa katika
picha ya pamoja na mgeni rasmi
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa), Profesa Elias
Jengo (kushoto) ambaye ni Mhadhili wa taaluma katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), aliyeko katikati ni Mkurugenzi wa
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana
,Utamaduni na Vijana, Profesa Hermas Mwansoko na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa
taasisi hiyo, Juma Bakari.Wengine ni baadhi ya wakufunzi
Kikundi cha sarakasi kutoka nchini Ethiopia kijulikanacho kwa jina
la Umoja kikionyesha umahiri wake wa kucheza
mtindo huo wakati sherehe za mahafali ya 23 yaliyoyofanyika
jana(juzi)s katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(TaSUBa)
iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani. Sherehe hizo ziliambatana na
Tamasha la 31 la Sanaa na Utamaduni.Picha na Maelezo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)