Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omari Kariati
akimsalimia Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwa Rais Mstaafu Ali Hassani
Mwinyi (kushoto), Mikocheni jijini Dar es Salaam. kabla ya hafla ya
wananchi wa Kata hiyo kukabidhiwa tangi la maji na kidanda cha
kujifungulia kina mama, iliyofanyika nyumbani hapo, leo.
Diwani Kariati akiongozana na Mzee Mwinyi na Mama Sitti Mwinyi kwenda eneo la tukio
UNAONA MAMBO YA KILIMO KWANZA? Akasema Omari Kariati wakati akitazama
maembe yaliyopo kwenye mwembe wa kisasa uliopo nyumbani kwa Mzee Mwinyi.
Kina mama wa Kwadelo wakiwa kwenye viwanja vya shughuli ya makabidhiano ya vifaa hivyo
"Kwanza tunamshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee wetu Ali Hassan
Mwinyi kwa kutukaribisha nyumbani kwake kukamilisha hafla hii. Shughuli
iliyotuleta hapa ni Mzee wetu kuwakabidhi wana-Kwadelo tangi kubwa la
maji la sh. 650,000 na kitanda cha kujifungulia kina mama, kisha
atamapatia sh. 200,000 kijana wetu aliyemuahidi kwa ajili ya kukamilisha
masomo yake ya ualimu pale Ununio" akasema Diwani wa Kwadelo Omari
Kariari kufungua shughuli. pembeni ni Mzee Mwinyi na Mkewe Mama Sitti,
wakimsikiliza.
Kisha mzee Mwinyi na mkewe wakasongea pamoja na waalikwa pahala vilipokuwa vitu vya kukabidhi. Hapa anakabidhi kitanda
Kwa furaha baada ya kukabidhiwa, mama mmoja wa Kwadelo akakifanyia majaribio kidogo kitanda hicho.
Kisha Mzee Mwinyi akakabidhi tangi la lita 5000 kwa Mwadham Msami
(kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerereng'ombe, palepale
Kwadelo. Naye Omari Kariati akishuhudia
Baada ya kurejea meza kuu, Mzee Mwinyi akakabidhi sh. 200,000 kwa
kijana, Kassim Omar kwa ajili ya kumalizia masomo yake ya ualimu Chuo
cha Ununio, Bagamoyo.
Kisha Mzee Mwinyi akaeleza yake ya moyoni kuwahusia wana Kwadelo na
Watanzania kwa jumla akisema "wanaodhani maandamano yanaleta maendeleo
wanapotea, maendeleo yanaletwa na kujituma na kutumia fursa zilizopo
kufanya kazi kwa bidiii". Kushoto ni Mama Sitti Mwinyi.
Picha za pamoja na Mzee mwinyi zikapigwa kwa makundi ya wananchi wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
Hawa ni kina mama wa Kwadelo wakiwa na Mzee Mwinyi
Na kina Baba wakachangamkia
Vijana wa Kwadelo wakiwa nyumna ya Mzee Mwinyi katika picha ya pamoja
Hawa pia ni vijana wa Kwadelo kati ya 50 wanaofanya shughuli zao jijini Dar, waliojitolea kwenda kulima katika kata hiyo
Waandishi nao wakatumia fursa hiyoo adhimu kupigapicha na Mzee Mwinyi. Kulia kabisa ni Mimi
Hapa pia ni waandishi wakichangamkia fursa hiyo.
"Karibuni Chai" akasema Mama Sitti kuwakawakabisha wageni mwishoni mwa shughuli
Wageni wakachangamkia chai.Picha Kwa Hisani Ya Francis Dande Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)