Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akifuatana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China
Hui Liangyu baada mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar
jana,akiwa katika ziara ya siku mbili.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akimkaribisha Makamo Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Watu wa China
Mhe,Hui Liangyu,mara alipowasili Ikulu Mjini Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisalimiana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China
Hui Liangyu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa katika ziara ya siku
mbili ,Makamo Waziri Mkuu Liangyu akiwa na ujumbe wake walifanya
mazungumzo na Rais
Waziri wa Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf
Mzee,kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini
Mkataba wa Mashirikiano ya Kiuchumi na Kiufundi,na Naibu Waziri
wa Biashara wa China ZHONG SHAN,kwa Upande wa jamhuri ya Watu wa
China,katika mashirikiano hayo Zanzibar itapatiwa RMB 60 Milioni sawa na
Fedha za Tanzania 14,8 Bilioni,ambapo fedha hizi ziatatumika katika
kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.
Waziri wa Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf
Mzee,kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akibadilishana
Mikataba baada ya kutiana saini Mashirikiano ya Kiuchumi na
Kiufundi,na Naibu Waziri wa Biashara wa China ZHONG SHAN,kwa Upande wa
jamhuri ya Watu wa China,katika mashirikiano hayo Zanzibar itapatiwa RMB
60 Milioni sawa na Fedha za Tanzania 14,8 Bilioni,ambapo fedha hizi
ziatatumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar
---
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China
leo zimetiliana saini Mkataba juu ya Mashirikiano ya Kiuchumi na
Kiufundi ambapo Zanzibar itapatiwa jumla ya RMB 60 Millioni sawa na
TZS,14.8 BILLIONI.
Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Waziri wa Nchi Fedha
,Uchumi na Mipango ya Maendelro Omar Yussuf Mzee ndie alietia saini na
kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Naibu Waziri wa
Biashara Zhong Shan ndie alietiana saini ambapo ulishuhudiwa na Makamo
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sief Ali Idd na kwa upande wa China
Naibu Waziri Mkuu wa nchi Hui Liangyu.
Kwa mujibu wa Mkataba huo wa Mashirikiano Zanzibar itafaidika katika
Ujenzi wa Majengo mapya na Ukarabati mkubwa wa Majengo yaliopo katika
Hospitali ya Abdulla Mzee ..Pia Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya
Mwananakwerekwe.Halkadhalika Zanzibar itafaidika katika utiaji wa Taa za
Barabarani zitakazotumia Nishati ya jua katika baadhi ya Barabara kuu
za Mjini.
Aidha Mkataba huo unaelezea kuwa Zanzibar itapata Mafunzo Mafupi na
Marefu katika Fani tofauti ambayo itapendekezwa na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar . Mbali na hayo pia kutakuwapo Uchimbaji wa Visima vya Maji
pamoja na maeneo mengine ambayo Nchi mbili zitakubaliana.
Pia ujumbe huo wa China umetiliana saini na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar juu ya msaada wa Wataalamu wanne(4) kutoka China ambao
watakuwepo Zanzibar kwa miaka miwili(2) ambao watawafundisha Mafundi wa
Mitambo wa Studio yakurushia matangazo ya Redio pamoja na kutoa Vifaa
mbali mbali kwa ajili ya Studio hiyo.
Ujumbe huo wa China ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu uliwasili Zanzibar
leo jioni na kupokelewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Idd pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar wakiwamo Mawaziri. Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu
pamoja na maofisa mbali mbali wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed
Shein jioni hiyo hiyo alikuwa na Mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa
China Hui Liangyu Ikulu ambapo walizungumzia juu ya Ushirikiano kati ya
Nchi zao.
Usiku huu Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd
Amemuandalia Chakula Naibu Waziri Mkuu wa China pamoja na ujumbe wake
huko katika hoteli ya Lagemma Nungwi.
Kesho asubuhi Naibu Waziri Mkuu wa China na ujumbe wake watatembelea
kanisa la Anglican Mkunazini na baadae kuelekea Beit el Ajaib na Jumba
la Wananachi Forodhani na kuelekea Uwanja wa ndege kwa kurejea Dar es
Slaam.
IMETOLEWA NA
IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)