Hayati Luteni
Kanali (mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia, aliyekuwa Mpambe wa Rais wa
kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa
pili wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Rais
wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na
Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu
cha maombolezo leo Keko, jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Luteni
Kanali
(mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia, aliyekuwa Mpambe wa Rais wa kwanza wa
Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan
Mwinyi. Marehemu amezikwa jana Septemba 6, 2012 katika makaburi ya Kisutu
jijini Dar es salaam.
Hayati Luteni
Kanali (mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia, akiwa kazini kama Mpambe wa
Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na
baadaye Rais wa pili wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ndugu jamaa na
marafiki wa Hayati Luteni Kanali (mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia Jana
Septemba 6, 2012 Keko, jijini Dar es salaam.Picha Zote na IKULU
--
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
Jenerali Davis Mwamunyange salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Luteni Kanali
(mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia, aliyekuwa Mpambe wa Rais wa kwanza wa
Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi.
Katika
salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Nimepokea kwa majonzi na
masikitiko taarifa za kifo cha Luteni Kanali Makwaia ambaye nimejulishwa kuwa
alipoteza maisha Jumanne, Septemba 4, mwaka huu, 2012, katika Hospitali ya
Jeshi ya Lugalo mjini Dar es Salaam.”
“Katika
miaka yote ya utumishi wa Jeshi na utumishi wa umma, Luteni Kanali Makwaia
alikuwa mwadilifu na mwaminifu kwa nchi yake, alikuwa na weledi wa kiwango cha
juu katika taaluma yake ya kijeshi na alikuwa mtiifu kwa viongozi wake.
Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu zangu za rambirambi kufuatia
kifo hiki,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Aidha,
kupitia kwako natuma salamu za pole nyingi kwa familia ya marehemu Makwaia
ambao wamempoteza baba na mhimili wa familia. Pia, kupitia kwako, natuma salamu
za rambirambi kwa maofisa na wapiganaji wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) ambao wamempoteza ofisa na mpiganaji mwenzao.”
Luteni
Kanali (mst) Makwaia alijiunga na Jeshi Machi 24, mwaka 1974, na alilitumikia
kwa miaka 23 na miezi tisa kabla ya kustaafu. Alikuwa Msaidizi wa Mpambe wa
Rais kati ya mwaka 1978 na 1981 na kuwa Mpambe wa Rais kwa miaka sita hadi
1987. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
6
Septemba, 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)