
Spika
wa Bunge. Mhe. Anne Makinda (wa nne kulia) akifuatilia kwa umakini
ratiba ya ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa
Jumuiya ya Madola (CPA) kabla ya ufunguzi rasmi unaofanyika leo Mjini
Colombo Sri, Lanka, aliye kushoto kwake ni Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho na Mhe. Zitto Kabwe na aliye kulia
ni Mhe. Mussa Azzan Zungu. Mkutano huo umefunguliwa rasmi leo na Rais wa
Nchi hiyo Mhe. Mahinda Rajapaksa
Mhe.
Zitto Kabwe akiteta jambo na Mbunge toka Uganda (hakufahamika jina mara
moja) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimundu Banda
(katikati) mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA
unaofanyika nchini Sri Lanka. Kulia ni Mhe. Hamad Rashid Mjumbe wa CPA
tawi la Tanzania.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa MNelum Pokuna
Mahinda Rajapaksa kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama
cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofunguliwa leo na
Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Aliye pembeni yake ni Mjumbe
wa CPA Tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishangaa jambo wakati wakiwa katika
mazungumzo na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende mara baada ya ufunguzi
rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka
Wajumbe wote wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi leo









No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)