Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa akiongea na waandishi wa habari mkoani iringa jana.
---
Mbunge
wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa
amesikitishwa kuona viongozi wakuu wa serikali kukaa kimya kutokana na
kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Msigwa amesema amesikitishwa sana na kifo cha Mwandishi mwangosi kwani hata kilipotokea yeye alikuwa safarini kuelekea Ujerumani lakini kwa kuufahamu mchango
mkubwa aliokuwa nao Mwangosi katika kutetea haki kwa wananchi wa
Iringa na tasnia ya habari ilimbidi ahairishe ili kuweza kutoa pole kwa
familia ya marehemu.
Ameeeleza
kuwa yeye kama mbunge amesikitishwa sana na kuona viongozi wakuu
wanchi kama rais kutozungumzia suala hili na haswa kwa viongozi wa
ngazi ya mkoa na wilaya ambao marehemu alikuwa akifanya nao kazi kwa
karibu sana.
“Nimesikitishwa
sana kuona kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa kuzidi kuwepo ofisini
kwa lile lilitotokea, mikono ya kamuhanda na mikono ya Said Mwema
imejaa damu, na mimi naungana na wanahabari kuugomea uongozi wa RPC
Iringa” alisema.
Ameongeza
kuwa anasikitiswa sana Meya wa manispaa wa Iringa Amani Mamwindi
kuhusika katika utoaji wa amri ya kuvunjwa kwa vijiwe vya wananchama wa
CHADEMA.“Meya ametoa amri ya kubomoa vijiwe vya chadema akieeza kuwa
ni amri ya jiji na kuacha jukumu lake kubwa la kuhakikisha kuwa
takataka za mji zinatolewa na kuhakikisha uchumi unaendelea na badala
yake kuhusika kubomoa vijiwe vya wanachama pamoja na kutoa bendera na
hatutaruhusu hali hii iendelee” aliongeza msigwa.
Kuhusu
yeye kutoonekana kuwajibika jimboni na kuwa na ziara nyingi za nje
Msigwa amesema haendi huko tuu kwa maslahi yake binafsi ila anafanya ili
kujifunza mambo mengi ambayo yatakuja kuwasaidia wananchi baadae
nahii inatokana na yeye kuwepo katika uongozi wa katika wizara
mbalimbali ambapo ziara hizo zina maslahi kwa jamii nzima.
Kutokana
na hali hiyo mbunge huyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi
katika mkutano utakaofanyika katika eneo la soko kuu kuanzia saa nane
kamili na kuongea na wananchi kuhusiana na mambo mengi yanayohusiana na
maendeleo ya jimbo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)