MATUKIO KATIKA PICHA MAZISHI YA MWANDISHI WA TANZANIA DAIMA AGNES YAMO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MATUKIO KATIKA PICHA MAZISHI YA MWANDISHI WA TANZANIA DAIMA AGNES YAMO

Baadhia ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, marehemu Agnes Yamo, tayari kwa ibada fupi ya mazishi, nyumbani kwao Kigurunyembe, mjini Morogor jana mchana. 
Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho mwa marehemu Agnes Yamo, kabla ya mazishi yake, yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kola, mjini Morogoro jana mchana.
Ndugu, jamaa na marafiki wakishusha kaburini jeneza lenye mwili wa marehemu Agnes Yamo, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kola, Kigurunyembe mjini Morogoro jana mchana.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media Limited, Absalom Kibanda akiweka mchanga kwenye kaburi la merehemu Agnes Yamo, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kola, Kigurunyembe mjini Morgoror jana mchana. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Free Media Limited, inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, wakiongozwa na Mhariri Mtendaji, Absalom Kibanda, wakiweka kwa pamoja shada la maua katika kaburi la marehemu Agnes Yamo. Agnes aliyekuwa mwandishi wa magazeti hayo, amezikwa jana mchana kwenye makaburi ya Kola, Kigurunyembe mjini Morogoro.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Agnes Yamo, baada ya kuzikwa katika makaburi ya Kola mjini Morogoro jana mchana.
Mwanasheria Mkuu wa serikali, Frederick Werema akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Agnes Yamo, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kola mjini Morogoro jana mchana.Picha zote na Joseph Senga

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages