Makamuwa
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimnadi Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Bububu, Hussein
Ibrahim Makungu (BHAA) wakati alipokuwa akizindua Kampeni za uchaguzi
mdogo wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Geji, mjini Unguja
jana.
Mbunge
wa Iramba Mwigulu Nchemba, akimvisha Skafu ya Bendera ya Tanzania,
Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Bububu, kupitia CCM, Hussein
Ibrahim Makungu (BHAA) ikiwa ni ishara ya heshima kuvua utambulisho
wake na kumtunuku mgombea huyo, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Geji, mjini Unguja jana.
Msanii
wa muziki wa Taarab, na mkurugenzi wa kundi la Taarab la Jahaz Modern
Taarab, Mzee Yusuph, akishambulia jukwaa kwa vibao vyake vya sebene la
Taarab, wakati wa sherehe za uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa
Jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Geji, mjini Unguja jana.
Mgombea
wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Bububu, kupitia CCM, Hussein
Ibrahim Makungu, akiwa katikati ya umati wa wanachama wa CCM,
akisebeneka nao kwa pamoja wakati wa Sherehe za za uzinduzi wa kampeni
za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Geji,
mjini Unguja jan.
Mashabiki
na wanachama wa CCM, wakishangilia na kufurahia hotuba ya Mhe. Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao kwenye sherehe za uzinduzi wa
Kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa
Geji, mjini Unguja jan.

Geji, mjini Unguja jana.
Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba, akizungumza na kutema cheche wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)