Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokelewa
katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakati akirejea kutoka nchini
Marekani na Uingereza kwa ziara ya wiki mbili.(Picha, Salmin Said-Ofisi
ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar
---
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amerejea
nchini leo tarehe 17/09/2012, baada ya kumaliza ziara yake ya wiki
mbili nchini Marekani na Uingereza.
Maalim Seif aliondoka nchini tarehe mosi mwezi huu kwa ajili ya
kuhudhururia mkutano wa kimataifa unaohusiana na masuala ya demokrasia
duniani, ulioandaliwa na taasisi ya National Democratic Institute katika
mji wa North Carolina nchini Marekani.
Baada ya kumaliza mkutano na makongamano yaliyoandaliwa na taasisi
hiyo, Makamu wa Kwanza wa Rais aliendelea na ziara yake katika miji ya
Washington na London ambako alikutana na kufanya mazungumzo na baadhi
ya viongozi wa nchi hizo, pamoja na viongozi wa wa taasisi
zinazoshughulikia sera za mahusiano ya kimataifa.
Akiwa mjini Washington, Maalim Seif alikutana na msaidizi Waziri wa
mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Bwana John
Carlson katika jengo la Wizara hiyo mjini Washington, kuzungumzia juu
hali ya maendeleo ya siasa na demokrasia Zanzibar.
Pia alikutana na uongozi wa shirika la misaada la Marekani USAID,
pamoja na kuzungumza na viongozi wa jumuiya ya wazanzibari wanaoishi
nchini Marekani.
Huko Uingereza Maalim Seif alikutana na mabalozi wa nchi za Afrika
pamoja na maveterani wa Uingereza, ambao walikutana kuzungumzia masuala
mbali mbali yanayohusu maendeleo ya Zanzibar tangu kuundwa kwa serikali
ya Umoja wa kitaifa.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)