MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA KITAIFA YAFUNGWA LEO MKOANI IRINGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA KITAIFA YAFUNGWA LEO MKOANI IRINGA

 Afisa Mwandamizi wa Mawasiliano kwa Umma wa SUMATRA, Maria Msellem, (kushoto) akitoa maelezo juu ya namna ya matumizi sahihi ya kufuata sheria za barabara kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara kwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipokuwa anatembelea banda la Posili usalama barabarani jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Iringa Ritha Motto Kabati(kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Meneja Mauzo wa Airtel, Kanda ya Nyanda usini, Beda Kinunda  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa. Airtel ndio wadhamini wa maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na RPC wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akipokea zawadi ya Airtel
kutoka  kwa Meneja Mauzo wa Airtel, Kanda ya Nyanda usini, Beda Kinunda  mara baada ya kutembelea banda la Airtel ambao ndio wadhamini wakuu wa wa wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa. Kulia ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Pereira Silima.
Wabunge wa Viti Maalum mkoa Iringa, Ritha Motto Kabati (kulia) na  Ckiku Alfan Abwao (kushoto) wakiwa katika viwanja vya Samora mjini Iringa hii leo katika ufungaji wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa.
 Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Malangali Mkoani Iringa, Steven Mligo(kushoto) akitoa maelezo juu ya namna ya matumizi sahihi ya kufuata sheria za barabara kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara kwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipokuwa anatembelea banda la Polisi usalama barabarani jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Ofisa wa Wizara ya Ujenzi, (kuli0 akitoa maelezo ya Wizra hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea banda hilo. Kushoto kabisa ni Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge
 Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Barabara TANROAD wakiwa katika banda lao
 Mkurugenzi wa Mipango wa TANROADS, Mhandisi, Jason Rwiza  (kushoto) akitoa maelezo ya taasisi hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea banda hilo. Kulia ni kabisa ni Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge
Mneja wa Mkoa wa Iringa wa Shirika la Bima la Taifa, (NIC) Ally Mohamed (kulia) akitoa maelezo ya taasisi hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea banda hilo. Wengine ni Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Ritha Kabati (kushoto) na Kamanda wa Trafiki, Kamishna Msaidizi Mohamed Mpinga.
 Afisa Mauzo Msaidizi wa ASAS, Stanley Nyamle (kushoto) akitoa maelezo juu ya namna ya matumizi sahihi ya kufuata sheria za barabara kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara kwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipokuwa anatembelea banda la Posili usalama barabarani jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
 Wanafunzi wakitumbuiza kwa nyimbo katika kilele hicho cha Wiki ya Nenmda kwa Usalama Kitaifa mjini Iringa hii leo.
Wabunge wa Viti Maalum mkoa Iringa, Ritha Motto Kabati (kulia) na  Ckiku Alfan Abwao (kushoto) wakifurahia jambo katika viwanja vya Samora mjini Iringa hii leo katika ufungaji wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa.
 Wasanii wa kundi la Mizengwe wakitoa burudani katika sherehe za ufungaji wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaofa Mkoa wa Iringa. Kulia ni Mkaguzi wa Polisi, Abel Swai.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Makampuni ya ASAS, Salim Abgri kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nebda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa. Abri pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Redio One na Capita Radio, Deogratius Rweiyunga kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nebda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mmwenyekiti wa Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Geita, Willson Msuka kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nebda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa
Baadhi ya madereva wa Pikipiki mkoani Iringa waliopatiwa mafunzo maalum ya uendeshaji pikipiki na kufaulu wakila kiapo cha utii wa sheria za barabarani mbele ya Mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akifunga rasmi maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa Mkoani Iringa leo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages