Beki
wa timu ya Mafunzo Ali Othman (kushoto) akiokoa hatari galini kwake
mbele ya mshambuliaji wa timu ya KMKM Tizzo Charles, katika mchezo wa
ufunguzi wa ligi Kuu ya Grand Malt uliofanyika katika uwanja wa amaan
timu ya Mafunzo imeshinda 1--0.
Na Ally Mohammed, Zanzibar
Pazia
la ligi kuu Zanzibar limefunguliwa jana kwa mechi mbili kuchezwa
katika viwanja viwili tofauti, kwenye uwanja wa Amaan kisiwani Unguja
Mabaharia wa KMKM walikutana na Mafunzo, ambapo mechi hiyo imemalizika
kwa Mafunzo kuchomoza na ushindi wa bao 1-0, bao la mafunzo likipatikana
katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza kupitia Mohammed Abdulrahman.
Huko kisiwani Pemba nako kilipigwa mechi moja ikiwakutanisha mabingwa
watetezi wa ligi hiyo, Super Falcon na Chipukizi ambapo kwa mara
nyengine tena Super Falcon ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika
michuano ya Kimataifa ( LIGI YA MABINGWA AFRIKA) wamezidi kuonesha
udhaifu baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa bila kutoka kwa
Chipukizi, hii ni mechi ya sita mfululizo Super Falcon wanaendelea
kupokea kipigo, wakianzia katika michuano ya BancABC Super 8, ambapo
walipoteza mechi zao zote 3 za hatua ya makundi, kabla ya kukubali
kipigo cha 3-1 kutoka kwa Jamhuri katika mechi ya ngao ya Jamii
iliyochezwa Septemba 1 mwaka huu katika uwanja wa Amaan, juzi wakicheza
na Coastal Union ya jijini Tanga katika mechi ya kirafiki, mchezo
uliochezwa uwanja wa Ngome, Fuoni, Wilaya ya Magharibi, Unguja
walifungwa 2-0.
Ligi
hiyo inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi mbili, katika uwanja wa
Amaan kisiwani unguja, Klabu ya Malindi ambao wamenunua daraja kutoka
kwa Miembeni SC watacheza na timu iliyopanda daraja msimu huu Bandari na
katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba washindi wa pili wa ligi
iliyopita, Jamhuri wakicheza na Duma, mechi zota zinatarajiwa kuanza saa
10:30 jioni.
Ligi
kuu ya Zanzibar, ambayo msimu huu inafahamika kwa jina la Zanzibar
Grand Malt Premier League kutokana na mdhamini kinywaji cha Grand Malt,
inashirikisha timu 12, huku timu 8 zikitoka kisiwani Unguja na timu 4
zikitoka kisiwani Pemba, timu zinazotoka kisiwani Unguja ni Bandari,
Chuoni, KMKM, Mafunzo, Malindi, Mundu ambao wamenunua daraja kutoka kwa
Miembeni United, Mtende iliyopanda daraja msimu huu na Zimamoto.
Kwa upande wa kisiwani Pemba ni Chipukizi, Duma, Jamhuri na Mabinwa watetezi, Super Falcon.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)