Khadija
Mnoga aka KIMOBITEL akiimba wimbo wake mpya "Mgeni" wakati wa utambulisho wake
rasmi wa kujiunga na Bendi ya Extra Bongo ndani ya New White House Kimara
Korogwe Dar es salaam.
Kimobitel
akiimba na Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki wimbo wake mpya unaokwenda kwa
jina la "Mgeni" ndani ya New White house wakati wa utambulisho wake
rasmi.
Comredi
Ally Choki aka Mzee wa Farasi
Kimobitel
akizikonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya Meeda Sinza usiku wa kuamkia leo
wakati aliokuwa akitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa maeneo ya Sinza na maeneo
ya jirani.
Makamanda
wa Extra Bongo wakiongozwa na Ally Choki mwenye Tsheti nyeupe mbele, kutoka
kushoto ni Banza Stoni, Kimobitel na mwisho kulia ni Rogert Hega aka Katapila
wakiimba wimbo mpya wa Hadija Mnoga aka Kimobitel.
Ally
Choki Mkurugenzi wa Extra Bongo akiimba kwa furaha wimbo wa "Mgeni" ulotungwa na
Khadija Mnoga (Kimobitel). Mwanamuziki
Khadija Mnoga (Kimobitel) wiki iliyopita alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa
Habari kujiunga na Bendi ya Extra Bongo akitokea bendi ya African Stars (Twanga
Pepeta) aliyoifanyia kazi kwa miezi kadhaa. Juzi
Ijumaa na Jana Jumamosi ndiyo zilikuwa siku rasmi za kutambulishwa kwa mashabiki
na wapenzi wa extra Bongo.











No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)