Koplo Isack Mkaguzi wa magari katika jeshi la polisi Trafiki akimhoji mmoja wa madereva wa magari makubwa wakati alipokuwa akikagua gari aina hili lililokuwa likitokea nchini Congo DRC ambako lilipeleka mafuta, kulia ni Tunu akishiriki katika zoezi la ukaguzi wa magari, kikosi cha Trafiki kinaendesha zoezi la ukaguzi wa magari yote na kuyapa stika maalum zinazonyesha kuwa yamekaguliwa katika kuadhimisha wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo mwaka hu kauli mbiu ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”
Ukaguzi huo umefanyika katika eneo la Ipogolo mjini Iringa kwenye barabara kuu ya Dar es salaam -Tunduma ambako maadhimisha hayo yanafanyika kitaifa
Koplo Isack Mkaguzi wa magari katika jeshi la polisi Trafiki akumuandikia Stika mmoja wa madereva wa Daladala mkoani Iringa mara baada ya kukagua gari hilo.
Stafu Sajenti Yohana Mjema akilikagua Roli lenye namba T 456 ADQ lililokuwa limebeba matofali katika zoezi la ukaguzi wa magari kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama Barabarani, kulia ni Afande Tunu akishiriki katika zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)