MWANAMITINDO FLAVIANA MATATA AKIPITA JUKWAANI
Imani Makongoro
……………………………………………..
MWANAMITINDO maarufu nchini,
Flaviana Matata ameendelea kung’ara katika fani hiyo baada ya kung’ara
katika maonyesho ya wiki ya Mavazi ya London, London Fashion Week.
Flaviana ambaye kwa sasa anaishi
nchini Marekani kwa shughuli hizo za maonyesho mavazi, aliwavutia sana
wadau wa maonyesho hayo na kumfanya mwanamuziki nyota wa kike
duniani,Stefani Joanne Angelina Germanotta maarufu kwa jina la Lady
Gaga.
Mwanamitindo huyo aliwasisimua
wadau wengi wa mitindo wakiwemo watu maarufu duniniani na kuendelea
kujizolea sifa na kutangaza jina lake na nchi yake pia.
Flaviana amekuwa akishiriki
katika maonyesho hayo tangu mwaka 2010, hata hivyo mwaka huu ameonyesha
kukomaa zaidi na kuweza kutawala jukwaa hilo.
Maonyesho ya mavazi ya mwaka huu
yaliwahusisha wabunifu wengi maarufu wa mitindo ambapo mmoja wapo ni
Vivenne Westwood Red Label ambaye anatamba duniani.
Pamoja na kuwepo kwa mbunifu
huyo, mbunifu Philip Treacy naye alifanya mambo makubwa katika maonyesho
hayo yaliyozinduliwa na Lady Gaga.
Flaviana alipewa heshima kubwa
ya kuvaa jaketi la mwanamuziki aliyekuwa mfalme wa muziki wa aina ya
Pop, marehemu Michael Jackson. Pia alivaa mavaz ya wabunifu maarufu kama
Mike Fast na Christopher Raeburn.
Kutokana na jinsi alivyowenga
kutamba katika maonyesho hayo, Flaviana alifanyiwa mahojiano na gazeti
maarufu duniani la Marekani, Wall Street Journal.
Flaviana ambaye ni Miss Universe
Tanzania wa mwaka 2007, aliweza kuipromoti nchi yake katika maonyesho
hayo kama alivyofanya katika mashindano ya Miss Universe ya mwaka 2007
kwa kushika nafasi ya sita kati ya warembo 10 walioingia fainali.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai
alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kuona Flaviana anaendelea kufanya
vyema katika fani hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)