Balozi wa Marekeni Alfonso Lenhardt akiwa katika picha ya pamoja na watu
wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanaopata huduma zao katika kituo cha
Alamano, cha mjini Iringa.Picha na Frank Leonard-Habari Leo
---
Mratibu wa Kituo hicho, Christopher Kunzugala alisema Jumuiya za Kuweka na Kukopa (SILC) katika kituo hicho zina hisa zenye thamani inayokadiriwa kufikia Sh milioni 200, huku hisa moja ikiuzwa kati ya Sh 500 na Sh 10,000 kwa wanachama wa vikundi 52 vilivyoanzisha jumuiya hizo.
Balozi Lenhardt alisema Watu wa Marekani kwa kupitia Mfuko wa Rais wa
Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) walianza kukisaidia kituo hicho
tangu kilipoanza kutoa huduma ya uangalizi na matibabu mwaka 2005,
“Kituo hicho si tu kwamba kinawapa watu fursa ya kupata huduma ya
upimaji na matibabu, lakini pia kinatoa huduma za uangalizi na misaada
kwa watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI,” alisema.
Alisema ushirikiano wao na kituo hicho umewezesha mpaka sasa Marekani
isaidie utoaji huduma ya uangalizi na misaada kwa watu watu 2,043
wanaoishi na virusi na watu 1,795 wanaopata huduma za matibabu kituoni
hapo.
Aidha alisema kupitia misaada ya Watu wa Marekani, programu za “Tunajali
na Pamoja Tuwalee”, wametoa mafunzo kwa waelimisharika majumbani 85.
Mkurugenzi wa Kituo cha Alamano, Maria Mikela alisema kituo kimejengwa
kupitia Programu ya Awamu ya Pili ya Mradi wa Tunajali unaofadhiliwa na
USAID.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)