……………………………………………………………
KAMPUNI ya mawasiliano nchini ya
Airtel imeahidi kuendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwa na
lengo la kukuza maendeleo ya vijana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana katika hafla fupi ya kukabidhi shilingi milioni tano pamoja na
fulana mia moja kama udhamini wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu
zenge kauli mbiu ‘tukuze utalii wa ndani kupitia michezo’, Afisa
Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema kuwa kampuni yake itaendelea
kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwemo riadha ili kukuza maendeleo
ya vijana.
“Udhamini wetu wa shilingi
milioni tano pamoja fulana mia moja katika mbio za Rock City mwaka huu
unalenga katika kusukuma maendeleo ya vijana kupitia michezo kwa
tunaamini kuwa michezo imekuwa ni chanzo kikubwa cha ajira duniani.
“Tunaahidi kuendelea kusaidia
michezo mingine kwa kuwa pia tunaamini kupitia michezo mbalimbali
tunaweza kutangaza vivutio vyetu vya utalii duniani. Mfano nzuri ni mbio
za mwaka huu za Rock City Marathon zitakazowakutanisha wanariadha
mbalimbali kutoka nchi jirani,” aliongeza Bi. Matinde.
Akipokea hundi na fulana hizo,
Mratibu wa mbio hizo kutoka katika kampuni ya Capital Plus International
(CPI), Bi. Grace Sanga aliishukuru kampuni ya Airtel kwa kuendelea
kusaidia mbio za Rock City na kuyahasa mashirikia na makampuni mengine
kuiga mfano wa kampuni hiyo.
“Tunaishukuru Airtel kwa msaada
wao kwa kuwa msaada huu utatusaidia tujiandae vizuri na Rock City
Marathon ya mwaka huu itakayofanyika Oktoba tarehe 28 katika uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza,” alisema Grace.
Grace alisema kuwa mbali na
Airtel wadhamini wengine ni pamoja na Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Parastal Pension Fund (PPF), Geita Gold Mine, African Barrick
Gold, Air Tanzania Company Ltd (ATCL), Mamlaka ya Taifa ya Mbuga za
Wanyama nchini (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Nyanza Bottles,
New Africa Hotel na New Mwanza Hotel.
Aidha, Bi Sanga aliwaasa
wanariadha kujitokeza na kuanza kujisajili ili kushiriki katika mbio
hizo na kusema kuwa fomu za usajili zinapatikana katika ofisi za uwanja
wa CCM Kirumba, ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo
katika jengo la ATCL ghorofa ya tatu, ofisi za Bodi ya Utalii jengo la
IPS ghorofa ya tatu, Dar es Salaam, na zinapatikana katika tovuti ya www.rockcitymarathon.blogspot.com.
CPI ilitangaza kuwa atakaeibuka
kinara katika mbio za kilometa 21 mwaka huu kwa wanaume na wanawake
atazawadiwa shilingi milioni moja na laki mbili wakati mshindi wa pili
ataweka mfuko shilingi laki tisa na mshindi wa tatu ataondoka na shilingi laki saba.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)