YAMETIMIA' MBUYU TWITE ASAINI YANGA, SIMBA WABAKI MIDOMO WAZI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

YAMETIMIA' MBUYU TWITE ASAINI YANGA, SIMBA WABAKI MIDOMO WAZI

Beki wa timu ya APR ya Rwanda, Mbuyu Twite, aliyesaini Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam,  akiweka Dole katika karatasi zake na mkataba baada ya kumwaga wino na Klabu hiyo leo na kuwaacha mjia panda Viongozi wa Simba, ambao tayari walikwisha tangaza kumsajili na kumtambulisha rasmi katika Siku maalu ya Simba 'Simba Day' na kutambulisha jezi No, 4 kuwa ndiyo ingekuwa jezi ya Beki huyo, jambo ambalo limeonekana na kujulikana ukweli leo hii baada ya mchezaji huyo kuweka mambo hadharaniu. Picha na Michuzi Blog
 Mbuyu Twite, akisaini mkataba wake na timu ya Yanga, le.

Beki wa timu ya APR ya Rwanda, Mbuyi Twite, aliyesaini Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam,  akikabidhiwa jezi yake mpya na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Binkrebu, leo wakati wa hafla fupi ya kumsainisha.
******************************
IKIWA ni siku moja tu baada ya Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage, kutoa malalamiko kuwa wanachezewa rafu na Mahasimu wao Yamga na kumtuhumu mtoto wa kigogo kuhusika kuwahujumu katika usajili wa beki wa Rwanda Mbuyu Twite,  uongozi wa Yanga umekuja juu na kumtaka Rage adhibitishe kauli yake ikiwa ni pamoja na kumtaja mtoto huyo wa kigogo.

Yanga wamefanya kweli kwa kuweka wazi suala la mchezaji huyo na kumsainisha na kuwaacha Mahasimu wao midomo wazi wasijue la kufanya juu ya Beki huyo baada ya Yanga kukamilisha taratibu zote za uhamisho wa kimataifa wa Beki huyo na kufuata taratibu.

Rage alitoa kauli hiyo juzi mpaka kumpelekea kumwaga chozi sambamba na kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Katiba,Sheria,Maadili na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ya shirikisho hilo kuikandamiza klabu yake.

Akizungumza na waandishi Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Twiga na Jangwani Katibu Mkuu Yanga,Selestine Mwesigwa, alisema kuwa wao wanajua Rage ni muugwana na ni mkubwa katika nchi hii wanajua atamtaja na kuleta vithibitisho juu ya hilo mapema bila ya kuambiwa muda.

Aidha Mwesigwa alitoa ufafanuzi juu ya suala la mchezaji Mbuyu Twite ambaye inasemekana Simba wamemsajili na kusema kuwa wao Yanga wamemsajili kwa kufuata na kuheshimu kanuni na sheria za Cuf,TFF na FIFA hivyo basi wao hawajakurupuka katika usajili wake.

“Wenzetu naweza sema wamekurupuka kwa kuwa hawajafuata sheria wakati ndugu yangu Rage anajua kanuni na Sheria kwa hili namshangaa sana.”alisema Mwesigwa.

Alisema wao wameanza kufanya mchakato wa kumnasa beki huyo toka Novemba mwaka jana kabla ya kuanza mazungumzo na Simba juu ya aliyekuwa beki wao Kelvin Yondan na kusema kuwa walimtuma Mjumbe wa kamati ya Utendaji Abdallah Binkrebu kumfuatilia toka kipindi hicho.

“Sisi huyu mchezaji tumemsaka toka muda mrefu kabla hata ya Kagame kuanza na mara baada ya kumalizika kwa Kagame tulikuwa tunaangalia kiwango chake na kikaturisha.

"Binkrebu akafunga safari na kwenda kuzungumza na uongozi wa timu yake ya Fc Lupopo ya Kongo na wala sio APR, Simba wao wamenunua mali ya wizi wakati sisi tumeenda kwa mwenye mali.

Aliongeza kuwa mara baada ya leo kupeleka majina ya timu yao TFF ndipo wataweka adharani mambo mbalimbali juu ya beki huyo ikiwa na mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo.

1 comment:

  1. Anonymous6:16 PM

    uwepo wa mbuyu twite utaimarisha defence ya yanga.msimu uliopita defence ilitugharimu sana.sasa hivi yanga haitalazimika kumpanga canavaro kila mechi kwani beki imekamilika.wenzetu wa simba wana tatizo la kupenda kusifiwa lakinib hawataki kubeba lawama pale wanapokosea.taratibu zipo basi zifuatwe badala ya kutaka kuchafua watu

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages