Mheshimiwa Balozi, akiwa kwenye picha ya pamoja na
Wawakilishi wa Benki ya KCB Tanzania LTD. Pili (Kulia), Balozi Peter
Kallaghe, (kwanza kulia) Dada Shose Kombe, Bwana James Agin, Dada Pamela
Baguma na Naibu Balozi, Mh. Chabaka Kilumanga
Wawakilishi kutoka Benki ya Biashara ya Kenya (KCB)
wakijiorodhesha kwenye Kitabu cha Wageni, walipo karibishwa kwenye Ofisi
za Ubalozi wa Tanzania na Mheshimiwa, Balozi, Peter Kallaghe na Naibu
wake , Mheshimiwa, Chabaka Kilumanga, kwa mazungumzo mafupi. Mhe.
Balozi, alitaka kufahamu madhumuni ya safari ya wawakilishi hao wa KCB
hapa nchini Uingereza, na kutaka kukutana na Wananchi wa Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki.
Benki
hiyo kubwa Afrika Mashariki, imepata mafanikio na maendeleo makubwa
yaliyopatikana kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ya kuweza kutuma na
kupokea Pesa kwa njia ya mtandao (Internet), Simu za mkononi na
nyinginezo kwa ghalama nafuu zaidi, kulinganisha na njia nyingine za
utumaji na kupokea fedha.
-
UBALOZI WA TANZANIA, LONDON, KWA NIABA YA BENKI YA
BIASHARA KENYA (KENYA COMMERCIAL BANK (KCB)) INAWAALIKA WATANZANIA WOTE
WAISHIO UINGEREZA, KUJA KUJUMUHIKA NA WENZAO WA AFRIKA YA MASHARIKI
KATIKA HAFLA FUPI YA UFUNGUZI RASMI WA SHUGHULI ZA BENKI YA KCB HAPA
NCHINI UINGEREZA, KWA WAISHIO UGHAIBUNI (DIASPORA).
HAFLA
HIYO FUPI YA UFUNGUZI AMBAYO ITAWAJUMUISHA WAAFRIKA MASHARIKI, INA
LENGO LA KUPANUA WIGO WA SHUGHULI ZA BENKI YA KCB HAPA UINGEREZA,
KUTANGAZA SHUGHULI ZA UTENDAJI WAKE KATIKA KUWASAIDIA WANANCHI WA
JUMUHIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI KATIKA KUWEKEZA KIBENKI, KUFUNGUA
AKAUNTI ZA AINA TOFAUTI, KUJIWEKEA AKIBA, NJIA MBALIMBALI ZA KUTUMA NA
KUPOTEKEA PESA KWA NJIA YA MTANDAO (INTERNET), KUTUMA PESA KWA KUTUMIA
SIMU ZA MKONONI (MOBILE PHONES), IPADS NA NYINGINEZO.
HALFA
HIYO FUPI, ITAFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI 4 AUGUST 2012, KUANZIA SAA
16:00pm, KWENYE HOTEL YA HOLIDAY INN, BLOOMSBURY, CORAM STREET, LONDON, WC1N 1HT
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)