MSHAMBULIAJI
Azam Fc, aliyeuzwa kwa Klabu ya Simba SC, Mrisho Ngassa, amegoma kuuzwa
bila kumshirikisha katika makubailiano ya Klabu hizo mbili na kufikia
muafaka kwa kufuata utaratibu.
Akihojiwa
na Kituo kimaja cha Redio cha jijini Dar es Salaam jana jioni, Ngasa,
alisema kuwa ameamua kutinga Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za
Wachezaji, ili kupinga kuuzwa kwake katika klabu hiyo, akitokea Azam FC
bila kuhusishwa.
Akizungumzia
juu ya jambo hilo, Ngassa amesema kwamba hajafanya mazungumzo ya aina
yeyote na Klabu ya Simba SC wala Azam FC juu ya uhamisho wake zaidi ya
kusikia taarifa za uhamisho wake katika vyombo mbalimbali vya habari na
mitandao ya kijamii.
“Mimi
sijui chochote, na sikatai kuhamishwa, kwa sababu mimi soka ni kazi
yangu na ninaweza kucheza popote, ila taratibu zifuatwe tu, mimi si Kuku
ama Samaki kwani bidhaa hiyo ndiyo inaweza kuuzwa kwa mapatano na mteja
tu na mteja akachukua na kuondoka zaketu”alisema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)