Soko la Samaki la
Kasanga.
Mazungumzo yakiendelea Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Rukwa
Emmanuel Kachewa, Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a, Mrs.
Katyega, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO
Maneno Katyega, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Katibu Tawala
Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo
Florence Mtepa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Uwekezaji wa
Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega Ofsini kwake jana alipotembelea
Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufuatilia miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo
alitembelea Soko la Samaki la Kasanga pamoja na kujionea maendeleo ya mradi wa
umeme kwenda Wilaya ya Nkasi.
Hakika ziara ya
Mkurugenzi huyo Msaidizi imekuwa ya mafanikio makubwa kwani baada ya kutembelea
Soko kubwa la Samaki la Kasanga na kujionea umuhimu uliopo wa nishati ya umeme
katika kuendesaha soko hilo ameahidi kupitia Shirika lake kuwa soko hilo
litapatiwa Jenereta kubwa mbili kila moja ikiwa na uwezo wa 50KV. Alisema kuwa
Umeme utakaozalishwa kutokana na Jenereta hizo utaweza pia kuhudumia Vijiji vya
jirani vinavyolizunguka Soko hilo.
Jitihada za kulipatia Soko hilo umeme
zimekuwa zikipewa msukumo mkubwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya ambae amekuwa akilifuatilia kwa karibu ambapo amefanikiwa kumpeleka
kiongozi huyo wa Tanesco hadi eneo la mradi huo ikiwa ni katika jitihada zake za
kutekeleza agizo la Mhe. Makamu wa Rais alipofanya ziara yake Mkoani Rukwa na
kutoa agizo kwa uongozi wa Mkoa ushirikiane na Tanesco kuhakikisha Soko hilo
linapatiwa umeme.
Akiwa Mkoani hapa Kiongozi huyo wa Tanesco alikuta
baadhi ya mapungufu katika utekelezaji wa mradi utakaopeleka umeme Wilayani
Nkasi ambapo walishauriana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambapo walikubaliana
litafutwe suluhu la changamoto hizo badala ya kulaumiana ili kukamilisha mradi
huo muhimu kwa Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa kwa
ujumla.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi
Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega (Kushoto) na Kaimu
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Rukwa Emmanuel Kachewa walipotembelea
Soko la Samaki la Kasanga jana.Picha na Habari na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa-Hamza Temba
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)