Bw.
Eric Berman Mkugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa inayohusika na
utafiti wa masuala ya silaha ( Small Arms Survey Poject) yenye makao
yake Geneva, Uswisi, akifafua jambo wakati wa uziduzi ya taarifa ya
utafiti uliofanyika mwaka huu. Mkurugenzi huyo ameonyesha nia ya
kushirikiana na Tanzania katika kufanya utafiti kuhusu juhusi za
Tanzania katika kudhiti silaha haramu. Amesema taasisi yake imevutiwa
sana na umakini wa tanzania katika zoezi hilo.
---
Na Mwandishi Maalum
Taasisi
inayotambuliwa na kuheshimika kimataifa kama chanzo rasmi cha utoaji
taarifa zinazohusu silaha, imeelezea nia yake ya kushirikiana na
Tanzania kufanya utafiti kuhusu zoezi la udhibiti wa silaha haramu.
Hayo
yameelezwa na Bw. Eric Berman, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo
ijulikanayo kama Small Arms Survey Project yenye Makao yake Makuu
Geneva, Uswisi, wakati alipokutana na kubadilishana mawazo na Meja
Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja
wa Mataifa.
“
Tunafahamu Tanzania ni kati ya nchi zilizomakini kwenye utekelezaji
wa zoezi la udhibiti wa silaha haramu, ikiwamo uwekaji wa alama
kwenye silaha. Kwa hiyo tungependa kufanya mazungumzo ya kuangalia
namna gani tunaweza kushirikiana nakufanya utafiti kuhusiana na juhudi
zenu hizi” akasema Bw. Berman.
Aidha
akaongeza kwamba hata wenzao kutoka Taasisi ya Kanda ya Afrika
Mashariki inayohusika na masuala ya silaha ndogo ndogo ( RECSA) pia
wamewadhibitishia kwamba Tanzania ni kati ya nchi makini.
Nia hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji Berman ya kutaka kushirikiana na Tanzania kufanya utafiti huo, imefuatia mchango alioutoa Meja
Ibuge kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa Mkutano wa pili wa
Mapitio ya Mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu silaha ndogo na nyepesi (
United Nations Program of Action).
Mkutano
huo ambao ni wa wiki mbili unafanyika hapa UM, na umefunguliwa siku
ya jumatatu wiki hii na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw.
Jan Eliasson. Madhumuni mkutano huu pamoja na mambo mengine ni
kutathimini mchakato wa utekelezaji wa mpango huo ambao nchi wanachama
waliupitisha kwa kauli moja mwaka 2001.
Katika
mchango wake, pamoja na mambo mengine, mjumbe huyo wa Tanzania katika
Mkutano huo, ameeleza kwamba Tanzania siyo tu imekuwa ikitekeleza kwa
vitendo zoezi la udhibiti wa silaha haramu, lakini pia inaendelea na
kazi kubwa ya uwekaji alama kwenye silaha, zinazomilikiwa na serikali
na zinazomilikiwa na watu binafsi.
“
Mwaka 2009, Serikali ya Tanzania ilianza zoezi la kuweka alama
kwenye silaha, hadi leo hii tayari tumeshaweka alama kwenye silaha
zaidi ya 38,000 zinazomilikiwa na serikali na zinazomilikiwa na watu
binafsi” akasema Meja Ibuge Na kuongeza kuwa zoezi hilo limehusisha
mikoa 12 ya Tanzania Bara na kwamba ni zeozi endelevu ambalo lengo
lake ni kuhusisha mikoa yote 30 nchini.
Akafafanua
zaidi kwamba serikali kwa kushirikiana taasisi za kikanda kama vile
RECSA na GZT imeendelea na jitihada za kuwajengea uwezo kwa
kuwapatia mafunzo mbalimbali maofisa wake.
“
Tumejidhatiti kuendelea na zoezi hili tukiamini kwamba hatimaye
taasisi za kikanda na kimataifa nazo zitaendelea kuchagiza juhudi hizi
pamoja na ushirikiano ili hatimaye sote kwa pamoja tufanikishe
kuondokana na biashara haramu ya silaha ndogo na nyepesi” akasisitiza
Ibuge.
Akizungumzia
kuhusu matumizi ya silaha haramu pamoja na usambazaji wake, Meja
Ibuge amesema, Tanzania inawasiwasi juu ya hali ya ongezeko la
utengenezaji, uhamishaji na usambazaji haramu wa silaha hizo ikiwa ni
pamoja na ulibikizaji usiodhibitiwa.
Aidha
akaongeza kwamba Tanzania inamashaka na kuwapo kwa mlundikano usio wa
uwiano wa mahitajio ya silaha husika kwa matumizi halali kati ya m
nchi zilizoendelea na zinazoendelea.
Akasema
ulundikaji huo wa silaha kukichangiwa na kutokuwapo kwa udhibiti wa
uzagaaji wake ni tisho kubwa kwa amani, usalama na maendeleo hususani
Barani Afrika.
Utafiti
ambao umefanywa na Taasisi ya Small Arms Survey project umeonyesha
kwamba kuna takribani silaha ndogo milioni 875 ambazo ziko kwenye
mzunguko duniano kote. Silaha hizo zimetengenezwa na makampuni zaidi ya
elfu moja kutoka karibu nchi100.
Aidha
ripoti ya utafiti huo ambayo ni ya mwaka huu wa 2012 na imezinduliwa
wakati wa Mkutano huu , imebainisha kwamba kumekuwapo na ongezeko la
dhamani katika uhamishaji wa kimataifa wa silaha ndogo na nyepesi,
kutoka dola 4 bilioni mwaka 2006 hadi dola 8.5 bilioni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)