SIMBA YACHAPWA 3-1 NA NAIROBI CITY STARS UWANJA WA TAIFA JIONI HII KATIKA TAMASHA LA SIMBA DAY - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SIMBA YACHAPWA 3-1 NA NAIROBI CITY STARS UWANJA WA TAIFA JIONI HII KATIKA TAMASHA LA SIMBA DAY

Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Nairobi City Stars katika mchezo wa kirafiki wa tamasha la Simba Day linalofanyika kwenye uwanja wa Taifa Tamasha hilo limeandaliwa na klabu ya Simba na hufanyika  kila mwaka Agosti 8 na kushirikisha timu marafiki wa klabu hiyo huku wachezaji na viongozi mbalimbali wakipewa zawadi kwa mchango wao kwa klabu hiyo, Katika mchezo wa leo, hivi sasa mpira umekwisha na Simba imefungwa magoli 3-1 na timu  ya Nairobi City Stars kutoka nchini Kenya

Hili ndilo benchi la ufundi la timu ya Nairobi  City Stars kutoka nchini Kenya
Benchi la ufundi la timu ya Simba kushoto ni kocha wa timu hiyo Bw. Milovan.
Kikosi cha timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa paambano hilo.
Kikosi cha timu ya Nairobi City Stars kutoka Kenya kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa paambano hilo.
Mchezaji wa timu ya Simba kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi wa pili kutoka kulia akiongozana na wachezaji wenzake.
Mashabiki wa simba waliojitokeza kuishangilia timu yao katika siku ya simba day.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages