JUMLA
ya warembo 13 wanataraji kupanda jukwaani kuwania taji la Redd’s Miss
Mwanza 2012, shindano litakalo fabnyika Ijumaa Agost 31, 2012.
Kwa mujibu wa taarifa ya Sisi Entertainments, inaeleza kuwa shindano hilo litafanyika katikaUfukwe mwanana wa Ziwa Victoria Yatch Club kuanzia majira ya saa 20:00 usiku. Miongoni mwa washiriki ni pamoja na Aisha Eddy(22),Stella Augustino, Mourine Festo (19),Samia Said (20), Pendo Simon(21),Connie Frederico (19), Stella Charles(23),Happiness Emmanuel(19),Rabia Msafiri(20),Mage Charles(19),Monica,Clara Nuru(18),Happiness Daniel(23).
Shindano hilo litapambwa na burudani kutoka kwa Malikia wa Mipasho Hadija Omar Kopa na mkongwe Mwanahawa Ally, pia msanii wa mziki wa Kizazi kipya na mkali wa Ragga na miduara Bob Haisa atahakikisha hapakaliki. Mrembo anayeachia taji ijumaa hii ni Irene Karugaba aliyekaa na taji hilo tangu mwaka Jana 2011.
Shindano la Redds Miss Mwanza 2012 limedhaminiwa na Redd’s original, Coco cola,Star Times,Radio Free Africa,Isamilo Lodge,Two Sisters Salon,Whitney Fashion,Mama Nyimbo Decoration, Photo Spot, Stopper Entertainment, Matunda Insurance,Ef Outdoor,Cxc Africa.
Viingilio ni shiling 20000 viti vya kawaida na 50000 kwa vip.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)