Katibu Mkuu wa ADC Lukas Limbu
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na tukio la
wananchi wa vijiji Bugatu, Misungwi na Mwabulunga kuvunjiwa nyumba na
kuchomwa moto kwa madai ya kuvamia na kuishi ndani ya Hifadhi ya taifa
ya Sakaya wilayani Magu Agosti 2, mwaka huu.
Philipo James akiwa amekaa
kandokando ya mabaki ya nyumba zake mbili zilizoteketezwa kwa moto na
anadai wake zake wawili wamemkimbia na kumwacha na watoto wake wanne
Moja ya famili ya mzee Manhe
Mayoka ikiwa imejifadhi katika kibanda kibovu ambacho hakijaezekwa baada
ya nyumba zao nne kuvunjwa na kuchomwa moto katika kijiji cha Bugatu
Magu wakidaiwa kuvamia na kuishi ndani ya hifadhi ya taifa Sayaka
kinyume cha sheria.
Mama akiwa hana la kufanya akiwa
katika kibanda abacho kimekuwa makazi yao kufuatia nyumba yao kuvunjwa
na kuchomwa moto ,hapa akiwa na watoto wake wawili.
Kijana akiingia katika banda ambalo wanalitumia kulala baada ya nyumba zao kuvunjwa huko Mwabulenga Magu juzi
Katibu wa ADC akiangalia moja ya
makaburi yaliyokutwa eneo linalodaiwa kuwa hifadhi ya taifa
Sakaya.Kaburi hilo ni la mwaka 1966 ambalo ni la moja ya familia
iliyovunjiwa nyumba 9 kwa madai ya kuvamia hifadhi hiyo
Katibu wa ADC , Lukas Kadawi
(mwenye suti nyeusi ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya familia
ya Ester Kihuruma (kushoto kwa katibu huyo wa ADC ) , alipokwenda kuwapa
pole wahanga wa tukio la kuvunjiwa nyumba zao wakidaiwa kuvamia hifadhi
ya Sakaya.
Mkuu
wa Wilaya ya magu, Jaqueline Liana akisistiza jambo kuhusiana na tukio
la kuvunja nyumba za wakazi wa vijiji vya Bugatu, Mwabulunga, salama,
Kitongo, Misungwi na Lugata wakidaiwa kuingia ndani ya hifadhi kinyume
cha sheria. Picha na Mashaka Baltazar wa Fullshangwe Mwanza
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)