kamanda Ras makunja na Award IDA.
FFU wa Ngoma Africa Band na TUZO za Kimataifa.
Ngoma Africa Band" aka FFU
---
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani
ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU watatingisha jukwaa la ALAFIA
Festival,mjini Hamburg,Ujerumani siku ya jumapili 26.8.2012 ,onyesho
hilo kubwa la wazi linafanyika katikati ya kitovu cha mji wa Hamburg,
eneo la Hamburg-Altona, ambapo
patakua na pata shika ya nguo kuchanika.
Ngoma Africa band inashikilia award ya
kimataifa " IDA-International Diaspora Award" kwa kuchaguliwa kuwa bendi
bora ya kiafrika inayowakilisha vizuri kimataifa na kuwanasa mamilioni
ya washabiki kila kona duniani,imetajwa mara nyingi kuwa bendi bora
katika maonyesho mengi ya kimataifa.
Kikosi kazi hicho kinachoongozwa na
mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras makunja wa FFU,kwa sasa
kinatamba na CD mpaya "Bongo Tambarare" ambayo inasikika katika kambi
yao at
www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)