Mwanafunzi wa Darasa la Saba shule ya msingi Hogolo, aliyefahamika kwa jina la Matha Mazoea Mwenye umri wa Miaka (14) ameuawa kwa kunyongwa na kufukiwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Sephen
alisema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11/08/2012 majira ya saa 08:00
asubuhi katika mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo Kata ya Hogolo tarafa ya
Zoisa Wilaya ya Kongwa.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi
kwani marehemu alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu
aliyejulikana kwa jina la Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano na mpenzi
wake mpya aliyefahamika kwa jina la Wilfredy Muhaha @ Kabo mwenye miaka
(17) “ Alielezea Kamanda Zelothe
Katika
tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu watatu
kwa tuhuma za mauaji hayo ambao ni Asha Jafari Mohamed mwenye umri wa
miaka 16, mkulima, mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa
marehemu na Rino Mazoea mwenye umri wa miaka 21, Mkulima, Mkazi wa Ikulu
Hogolo Wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Bw. Zelothe alieleza kwamba ili kufanikisha uchunguzi wa awali Jeshi la Polisi pia Wilayani humo linamshikilia mpenzi mpya wa marehemu Bw. Wilfredy s/o Muhaha pamoja na kumtafuta mpenzi wa zamani wa marehemu Bw. Heri s/o Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa.
Aidha kamanda Zelothe alisema Katika tukio hilo Kaka wa marehemu ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakuweza kutoka usiku huo ili kushuhudia nini kinaendelea.
Kamanda
Zelothe alisema Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo
Kijijini na kwamba siku ya tukio walikuwa wameondoka kwenda katika
Vijiji vya jirani, ambapo bibi yake na marehemu alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda kijiji cha Banyi banyi kwa Shughuli za kutemebelea wagonjwa.
Wakati
huo huo Gari lenye namba za usajili T. 750 AEU aina ya TOYOTA CHASER
likiendeshwa na Kenedy James mwenye umri wa miaka 48, Mkazi wa Mpwapwa
liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha Salum Kaduma mwenye
umri wa miaka (13) Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Katika shule ye
sekondari ya Mpwapwa, na kusababisha kifo chake.
Mkuu
huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma alisema ajali hiyo ilitokea
mnamo tarehe 12/08/2012 majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la
Kisima Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa
magurudumu mawili ya upande wa kulia kitu kilichopelekea gari hilo
kuacha njia na kupinduka.” Aliongeza Bw. Zelothe
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)