Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na uongozi wa
Kiwanda cha Bia cha Tanzania (TBL) uliomtembelea ofisini kwake leo ukiwa
na lengo la kuwekeza kwenye kilimo cha shairi ambayo ni malighafi
muhimu katika kiwanda hicho cha kutengeneza bia nchini. Mkoa wa Rukwa
una ardhi yenye rutuba kustawisha mazao mbalimbali ya kilimo ikiwemo
mchele, mahindi, maharagwe, ngano, alizeti, mtama, ulezi n.k. Katika
kuwekeza kwao wataanza kwa kushirikiana na wakulima wadogowadogo ambao
wapo Mkoani Rukwa kwa kuwawezesha zana bora za kilimo hicho pamoja na
pembejeo ambapo pia watamiliki mashamba yao wenyewe kwa ajili ya kilimo
hicho.
Ndugu
Gerry Van Den Houten ambaye ni Mkurugenzi wa Usambazaji wa Sabmiller ya
South Africa ambayo ina mashirikiano na TBL akielezea lengo na faida za
uwekezaji huo ambao licha faida kubwa itakayopatikana pia itatoa ajira
kwa vijana wengi Mkoani Rukwa pamoja na kuhamasisha kilimo cha zao hilo.
Kulia kwake ni Bennie Basson ambaye ni Menenja wa Shairi wa kiwanda
hicho cha bia cha Tanzania (TBL).
Timu
ya Uongozi wa TBL ambayo pia ilikuwa imeongozana na baadhi ya wakulima
wadogowadogo wa shairi Mkoani Rukwa wakiwa Ofsini kwa Mkuu wa Mkoa huo
kwenye mazungumzo juu ya uwekezaji huo.Picha
ya Pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, baadhi ya viongozi wa Mkoa na
Viongozi wa TBL uliombatana na baadhi ya wakulima wadogowadogo wa shairi
Mkoani Rukwa. (Picha na Hamza Temba-Rukwareviw blog-Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa Rukwa)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)