Mkuu
wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua maoni
kutoka kwa Mhasibu wa Wizara ya Fedha Abbas Myeto(kulia)kuhusu
taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wa umma wanapostaafu . Mkuu
huyo wa Nkoa wa Singida aliomba ufafanuzi huyo leo alipotembelea banda
la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane
yanayoendelea mjini Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua jana mjini
Dodoma kutoka kwa watendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini
(GPSA) kwanini kuna utofauti wa ubora katika bendera ya Taifa ya kuweka
katika magari kwa viongozi. Mkuu Mkoa huyo aliuliza swali hilo leo
alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima
kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma. Aliyeshika bendera ndogo
ya taifa ni Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai
Mato (kulia).
Mkuu
wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi
jinsi Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] inavyosaidia
katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa yakifanyika
kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi za
serikali na taasisi zake. Mkuu Mkoa huyo alipata maelezo hayo kutoka kwa
Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia)
jana alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya
wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
Mchambuzi
wa Mifumo ya Komputya Mkuu Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti ya
TEKNOHAMA ya kifedha , Wizara ya Fedha Margethi Ambrosi Nembo (kushoto)
akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia)
leo mjini Dodoma jinsi kuingiza mishahara na malimbikizo ya watumishi wa
umma kwa kutumia TEKNOHAMA . Mkuu Mkoa huyo alikuwa katika maonyesho ya
wakulima nanenane mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto
kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo
itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri
ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini.
Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipotembelea banda la
Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini
Dodoma. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)