MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS YAANZA NAIROBI LEO‏ - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS YAANZA NAIROBI LEO‏

Manchester United’s Marketing Director Jonathan Rigby (Right) hands over a replica shirt to Kenya’s Prime Minister, Right Hon. Raila Odinga (left) During the launch of Airtel Rising Stars Africa Championships in Nairobi. He was accompanied by Manoj Kohli CEO (International) & Joint MD, Bharti Airtel and Airtel Africa, Chief Marketing Officer, Andre Beyers (extreme right).
Arsenal’s Marketing Director Angus Kinnear hands over a replica shirt to Kenya’s Prime Minister, Right Hon. Raila Odinga During the launch of Airtel Rising Stars Africa Championships in Nairobi. The tournament which brings together Africa’s best talent in the boys and girls under 17 categories will take place from the 21st to the 25th of August.

Michuano ya Airtel yaanza Nairobi

Ndio program kubwa ya soka barani Afrika, Ilianzia kwenye ngazi ya wilaya mpaka Taifa kwenye nchi 15, ikijumuisha shule 18,000 na wachezaji 324,000 – wavulana na wasichana, Bingwa kushiriki cliniki ya Arsenal na Manchester United itakayofanyika Nairobi na Accra.

Nairobi, Kenya August 21st, 2012….. Michuano ya Airtel Rising Stars barani Afrika imetimua vumbi   Jijini Nairobi, Kenya. Michuano hiyo imeleta pamoja wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba na itaendelea mpaka Agosti 25.


Michuano hiyo ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya mpaka Taifa na kufanyika kwenye nchi 15 barani Afrika. Huu ni mpango kabambe wa Airtel Rising Stars, wenye lengo la kuwapa vijana chipukizi fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Ikiwa ni ya moja ya michuano mikubwa kabisa barani Afrika, jumla ya timu 18,000 zilishiriki na wachezaji 324,000 – wavulana na wasichana kushiriki. Hii ndio mara ya kwanza kushirikisha wasichana.


Michuano hiyo ilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Kenya, Mh Raila Odinga – akisindikizwa na Mtendaji Mkuu wa Bharti Airtel Afrika – Manoj Kohli


Michuano hiyo pia itaashiria uzinduzi wa kliniki mbili za soka za kimataifa zitakaozoendezwa na makocha kutoka klabu kubwa duniani – Arsenal na Manchester United – zote za Uingereza. Kwenye uzinduzi wa michuano hiyo pia walikuwa waakilishi kutoka kwenye Klabu hizo – Mkurugenzi wa Masoko kutoka Manchester United Jonathan Rigby na Mkurugenzi Masoko kutoka Arsenal Angus Kinnear. Uzinduzi wa kliniki utafanyika na wachezaji wa zamani wa Manchester United Peter Schmeichel na Ray Parlour kutoka Arsenal.


Kwenye mechi za ufunguzi, timu ya wasichana ya Kenya ilishushia kipigo cha magoli 11 wenzao wa Malawi wakati kwa upande wa wavulana Malawi ilishinda 5- dhidi ya Kenya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages