Msafara
wa Matembezi ya hisani ukiongozwa na Brass Band ya JKT Makutupora
kuelekea kanisa katoliki Dodoma kushiriki zoezi la changizo kwa ajili ya
ujenzi wa jengo la makazi la watawa wa shirika la Mt. Gema wa Galgani
jimbo Katoliki Dodoma. Msafara huo ulimuhusisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Dr. Rehema Nchimbi, Askofu wa Jimbo Katoliki Dodoma Mhasham Gervas
Nyaisonga watawa na wananchi wa kawaida.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati walio mstari wa mbele)
akishiriki zoezi la matembezi mapema leo hii wakati wa changizo kwa
ajili ya ujenzi wa jengo la makazi la watawa wa shirika la Mt. Gema wa
Galgani jimbo Katoliki Dodoma, kushoto kwake ni Askofu wa Jimbo Katoliki
Dodoma Mhasham Gervas Nyaisonga na kulia kwake mkuu wa shirika hilo
Sister Florence Mbeyu.
Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashsriki Mhe. Samuel Sitta ambaye alikuwa
Mgeni rasmi kwenye zoezi la harambee ya ujenzi wa jengo la makazi la
watawa wa shirika la Mt. Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma
akimsalimu kwa kumbusu Askofu mstaafu wa kanisa Katoliki jimbo hilo
Mhasham Martias Isuja.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) akimkabidhi Askofu
mstaafu wa kanisa Katoliki jimbo la Dodoma Mhasham Martias Isuja hati
maalum ya upendo wa Kweli kutoka kwa shirika la Watawa la Mt. Gema wa
Galgani jimbo Katoliki Dodoma, anayeshuhudia katikati ni mkuu wa shirika
hilo Mtawa Florencia Mbeyu.
Baadhi
ya akina mama wanaofaidika na huduma zinazotolewa na shirika la Mt.
Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma waliohudhuria zoezi la changizo
kwa ajili ya ujenzi wa jengo la makazi la watawa wa shirika hilo mapema
leo hii katika viwanja vya kanisa Katoliki jimbo la Dodoma.
Baadhi
ya watawa wa shirika la Mt. Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma
wakiwa wamekaa mbele ya jengo la makazi la watawa wanalolijenga wakati
zoezi la changizo kwa ajili ya ujenzi huo mapema leo hii katika viwanja
vya kanisa Katoliki .Picha Kwa Hisani ya Dodoma-yetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)