MAKARANI WA SENSA WALETA VURUGU WAKIDAI POSHO ZAO ZA SEMINA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKARANI WA SENSA WALETA VURUGU WAKIDAI POSHO ZAO ZA SEMINA

Makarani wa sensa  kituo cha shule ya sekondari mansipaa ya Kinondoni wakiimba wimbo wakutaka kulipwa posho za semina  ya siku saba kiasi cha shilingi 245,000 ambapo madai yao ilikuwa walipwe  leo lakini mpaka sasa bado hakuna hata mmoja ambae amelipwa.
Afisa wa sensa ambaye hakutaka jina lake litajwe akiongea na makarani wa sensa nakuwataka walipwe kiasi cha nusu ya posho ambayo ni shilingi 140,000,hata hivyo makarani hao waligoma wakidai kulipwa posho zao zote ndipo waingie kazini,
 Waandishi wa habari wakimhoji afisa wa sensa kutaka kujua chanzo cha vurugu hizo.
Makarani wa sensa wakiwa wamelizingira gari la afisa wa sensa kushinikiza kulipwa posho zao.
Makarani wa sensa wakipata changamoto kutoka kwa maafisa wa polisi walipofika katika eneo hilo kutaka kujua lini watalipwa posho zao.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages